HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 11 March 2019

ABDALLA SHAIBU 'NINJA', TINOCO WASIMAMISHWA MECHI TATU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
SHIRIISHO la mpira wa miguu nchini (TFF) kupitia Kamati ya Nidhamu ya TFF imetoa hukumu baada ya kuwatia hatiani wachezaji wa Abdallah Shaibu na Benedict Tinoco kwa kuwakuta na hatia ya kutenda makosa ya utovu wa nidhamu.

Kamati ya nidhamu imemkuta na hatia Ninja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu (TPL) na Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.

Katika maamuzi mengine Kamati ya nidhamu ya Nidhamu ya TFF, imemtia hatiani Mchezaji wa Mtibwa Sugar Benedict Mlekwa Tinoco kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa timu Biashara United Fc aliyekuwa ameanguka baada ya kuchezewa rafu, Kamati imempa adhabu ya kufungiwa kutocheza mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.

Mbali na hilo, Kamati pia imetoa maamuzi kwenye mashauri mengine kwa Simba na Yanga wote wakipigwa faini kwa makosa waliyoyafanya katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha Februari 16 mwaka huu.

Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa kulikuwa na vitendo vya ajabu katika mchezo huo kitu ambacho kilipelekea kamati ya masaa 72 kukaa na kutoa maamuzi juu ya Vilabu hivyo.

Kwa upande wa Klabu ya Yanga imepigwa faini ya milioni 6 kwa kosa la kuingia Uwanjani kwa mlango usio rasmi pia kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji kukaguliwa wakiwa koridoni.

Klabu ya Simba pia imepigwa faini ya milioni 3 kwa kuingia Uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad