HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 28, 2019

YANGA YATUA MWANZA KUIKABILI ALLIANCE SIKU YA JUMAMOSI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSIcha Yanga kimewasili mkoani Mwanza mapema asubuhi ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Alliance ya jijini humo utakaochezwa siku ya Jumamosi.

Yanga watacheza mchezo wa 26 wa ligi kuu baada ya kutoka kucheza mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Namungo na kufanikwia kutinga hatua ya nane bora.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa mchezo huo ni muhimu sana kwao na kuhakikisha wanaondoka na alama tatu ili kujiweka zaidi kwenye uongozi wa ligi.

Amesema, mchezo huo dhidi ya Alliance ni mgumu sana ila wachezaji wake wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo na watajituma kufanikisha wanawapa furaha mashabiki wa timu hiyo.
Yanga imesafiri na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na benchi la ufundi wakiongozwa na viongozi wa timu hiyo na watacheza mechi mbili katika kanda ya ziwa.

Kwa upande wa benchi  la ufundi wa Alliance wao wamejizatiti kuhakikisha wanabakisha alama tatu katika Uwanja wa nyumbani ikiwemo na kuonesha mpira safi kwa wanajangwani hao.

Kocha mkuu wa Alliance, Malale Hamsini amesema wanatambua ushindani uliopo na namna kikosi cha Yanga kilivyo bora ila kazi yao ni moja tu kubeba alama tatu ingawa anafahamu uzoefu waliokuwa nao.


"Tayari kwa sasa vijana wameshajibu na mfumo umeanza kueleweka na ndo maana unaona tunapata matokeo chanya, tunaiheshimu Yanga kutokana na uzoefu wao lakini tumejipanga kubeba pointi tatu nyumbani.

Alliance wataikaribisha Yanga ambao ni vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza michezo 25 huku wao wakiwa nafasi ya 7 na wakiwa wamekusanya pointi 36 baada ya kucheza michezo 28.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad