HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 13 February 2019

WIZARA YATOA MASAADA WA KISAIKOLOJIA KWA FAMILIA ZILOATHIRIKA NAMATUKIO YA MAUAJI NJOMBE

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii imetembelea kuwapa pole na kutoa msaada wa kisaikoloji na kijamii kwa Familia zilizoathirikana mauaji ya Watoto yalitokea mkoani Njombe.

Timu hiyo imetembelea  Familia ya Bw. Gorden Mfugale inayoishi Mtaa wa Joshoni Kata ya Mji Mwema Halmashauri ya Mji Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto mmoja wa kiume Gidrack Mfugale (5) aliyepotea tarehe 04/02/2019 na kupatika tarehe 10/02/2019 akiwa amefariki dunia huku kiganja cha mkono kikiwa  na  mwili wake ulikutwa na majeraha kichwani katika  eneo la Shule ya Sekondari Njombe.

Akizungumza katika ziara hiyo Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa Wizara imeamua kujumuika na wanafamilia hao kwa kuja kuwapa msaada wa kisaikolojia na kijamii ili kuondokana na msongo wa mawazo unaotokana na tukio lililompata Mtoto wao.

"Tumeguswa sana na msiba huu na matukio ya mauaji  yaliyotokea na kwa niaba ya Wizara tunawapa pole kutokana na majanga haya na tuko pamoja kuhakikisha mnapata msaada muhimu ya kisaikoloji na kijamii" alisema

"Na Wizara haitowatembelea ninyi tu bali Timu ya Wataalam wengine wa Wizara na Mkoa wapo katika familia nyingine huko wakifanya haya tunayoyafanya hapa" alisema

Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Rehema Kombe amesema kuwa msaada wa kisaikolojia na kijamii ni muhimu sana kwa familia zilizokumbwa na matatizo hayo ya mauaji ya watoto kwani familia zimekumbwa na taharuki kubwa.

“Suala la hili la msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa wanafamili hizi ni muhimu sana kwa watu hao na tutawasaidia sana ili kuondokana na msongo wa mawazo unaotokana na vitendo walivyofanyiwa watoto wao" alisema

Pia Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Njombe Bi. Teresia Yomo amesema kuwa mkoa umejipanga kuendelea kuzitembelea familia zote kwa kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri zote za Wilaya ya Njombe ili kutoa msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa familia zote sita zilizopatwa na matukio haya ya mauaji ya watoto wanane mkoani Njombe.

Kwa upande wake Bw. Gorden Mfugale aliyepoteza mtoto wake Gidrack Mfugale (5) amewashukuru wataalam hao kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wameona umuhimu wa kuwasaidia ili kuomdokana na msongo wa mawazo unaotokana na vitendo walivyofanyiwa watoto wao.

“Asanteni sana kwa kuja kutuona na kutupa pole na tunashukuru kwa kutuletea masaada wa kisakolojia na kijamii utatusaidia sana kurudi katika hali yetu ya kawaida sio kwangu tu hata kwa familia nyingine zilizokubwa na matatizo kama yetu” alisema.

Wizara ya  Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii ipo mkoani Njombe kwa kushirikiana na Wataalam wa Mkoa huo katika jitihada ya kutoa msaada wa Kisaikolojia na kijamii kwa familia zilizoathirika na matukio ya mauaji ya watoto mkoani Njombe.
 Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu(mbele) akiongoza timu hiyo na ya wataalam kutoka Mkoa wa Njombe kuitembelea familia ya Bw. Gordeni Mfugale  iliyopoteza Mtoto mmoja katika mauaji 8 yaliyotokea Mkoani Njombe   wakati Wataalam hao walipoitembelea familia hiyo leo.
 Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu (wa tatu kulia) akizungumza na familia ya Bw. Gordeni Mfugale iliyopoteza Mtoto mmoja katika mauaji 8 yaliyotokea Mkoani Njombe wakati Wataalam hao walipoitembelea familia hiyo leo.
Golden Mfugale(wa pili kushoto) aliyopoteza Mtoto mmoja katika mauaji 8 akizungumza na Timu ya Watalaam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wataalam kutoka Mkoa wa Njombe wakati Wataalam hao walipoitembelea familia hiyo leo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano W

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad