HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 4 February 2019

Wema Sepetu ndani ya Filamu ya Enemy Cops

Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MCHAMBUZI wa filamu nchini Zamaradi Mketema atambulisha ujio wa filamu yake mpya inayoitwa jina la Cops Enemy. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Zamaradi amesema filamu hiyo ina ubora kutokana na kuweka vionjo mbalimbali ambapo havikuwepo katika filamu zingine. Amesema uandaji  wa Filamu hiyo umegharimu  Sh.milioni 200 hadi kukamilika kwa filamu hiyo.

"Tumeshirikisha wasanii wa nchi tofauti Tanzania akiwemo msanii Wema Sepetu,Aunt Ezekiel na kwa nchi ya Nigeria akiwemo Van Vicker.

Aidha amesema filamu hiyo imeandaliwa  zaidi ya miaka miwili kutokana na kupatikana kwa watayarishaji (DIRECTOR) kutoka Australia ambae ni mahiri na ambaye ataungana na  Neema Ndepanya ambae ni Meneja wa Msanii Wema Sepetu. Zamaradi amefafanua zaidi filamu hiyo itawezwa kuangaliwa na rika za watu wazima kutokana na maudhui mengine si sahihi kwa mtoto kutazama .

Pia Zamaradi ametoa wito kwa wasanii kutengeneza filamu ambazo zitaweza kuingia kwenye tuzo za nchi za nje na kuifanya tasnia kuongeza uwigo wa kupata masoko nje za nchi. Kwa upande wake mtayarishaji wa filamu hiyo hapa nchini Neema Ndepanya amesema filamu ya Cops Enemy ni nzuri na ina mafundisho mengi kutokana na maudhui mengi kugusa hadhira katika jamii nyingi nje na ndani ya nchi.

Ndepanya ameeleza kuwa filamu imewapa vipaumbele kwa watu wote ambao wanaojua lugha ya Kiswahili na Kingereza kuwepo kwa mandishi yanayotafsiri maongezi katika filamu hiyo (Subtitle)

Pia ameeleza uwezo wa Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walionyesha kwenye filamu hiyo kutokana na kutumia lugha ya kiswahili zaidi ambapo uwezo wa Wema Sepetu ni wazi anajulikana kwa ustadi wake wa kutumia lugha ya kingereza hivyo kwa mara ya kwanza ametumia lugha ya Kiswahili zaidi.

"Wema Sepetu bado anatumikia adhabu yake aliyopangiwa na bodi ya filamu hivyo kuzinduliwa kwa filamu hiyo hakutoathiri chochote isipokua alipewa nafasi ya kufanya kazi zake ambazo adhabu hiyo kabla ya kutolewa alikua akiziandaa ndio maana wema Sepetu ametajwa kwenye tuzo za Sinema Zetu na kisheria ana haki ya kushiriki kutokana na tuzo hizo zilishamtangaza kabla ya kupewa adhabu hiyo" amesema Ndepanya.

Pia ametoa shukrani za dhati kwa mmiliki wa filamu hiyo zamaradi Mketema kwa kuweza kumuamini na kulifanikisha hilo kwani ameweza kujifunza vingi jinsi ya kuandaa filamu kwa viwango vya hali ya juu kutoka kwa watayarishaji wa nchini Australia na Nigeria.
Mchambuzi wa filamu nchini, Zamaradi Mketema akizungumza na waandishi wa habari wakati akitambulisha ujio mpya wa filamu yake ya Cops Enemy jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad