HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 14, 2019

WAZIRI LUGOLA ATAKA ASKARI WAPANDISHWE VYEO, WAREKEBISHIWE MISHAHARA, WALIPWE FEDHA ZA UHAMISHO NA LIKIZO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, jijini Arusha leo, kuhusu masuala mbalimbali ya watumishi hao. Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Sehemu ya askari na watumishi raia wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo pichani), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, jijini Arusha leo, kuhusu masuala mbalimbali ya watumishi hao. Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Askari wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Arusha, CP Meshaki akizungumza katika Mkutano aliouhitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani). Askari huyo alimuomba Waziri huyo atatue changamoto mbalimbali zinazowakabili mkoani humo. Hata hivyo Waziri Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake (hawapo pichani), jijini Arusha leo, kuhusu masuala mbalimbali ya watumishi hao. Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Longinus Tibishubwamu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara, MOHA-Arusha.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara yake nchini, wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo. Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili kupandishwa na kurekibishiwa mishahara, kwa kuwa Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli askari hao wana haki kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, jijini Arusha leo. Lugola alisema katika uongozi wake hataki kusikia askari wananyanyaswa, na pia changamoto hizo zinapunguza nguvu ya utendaji kazi wa askari hao wanaofanya kazi ngumu. Lugola alisema alitoa agizo la askari wanaostahili kupandishwa cheo, kurekebishiwa mishahara yao, wanaodai kulipwa fedha za uhamisho pamoja na changamoto mbalimbali zingine alizozielekeza, ziwe zimetatuliwa tangu mwaka jana, hata hivyo amesema kwa wale wenye sifa amewataka askari hao wamuamini kwakuwa watapewa vyeo vyao hivi karibuni.

“Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini, lakini naamini kila kitu kinaenda vizuri na ahadi niliyoitoa itakamilisha kwa wale askari ambao wanasifa watapewa vyeo hivi karibuni,” Alisema Lugola. Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli anatoa mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna upungufu mkubwa wa nyumba hizo.

“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,” alisema Lugola. Pia Lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi. Lugola alisema jambo ambalo linamuumiza kichwa ni kuhusu madai ya askari na watumishi wa wizara yake ambayo anasema kama wafanyakazi hawatalipwa haki zao na utendaji wa kazi utapungua. Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kikazi na tayari amemaliza ziara yake Makao Makuu ya Mkoa na leo yupo Wilaya ya Arusha, na baadae ataenda Wilaya ya Meru, Arumeru, baadaye Longido, Monduli, Karatu na ataimaliza ziara yake akiwa Wilaya ya Loliondo mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad