HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 14, 2019

Shirika la Railway Children latoa mafunzo kwa waandishi wa habari

SHIRIKA la Railway Children limekutana na waandishi wa habari katika warsha maalumu wa  kutolea  ufafanuzi kuhusu mazingira wanayoyapitia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na kutoa mafunzo kuhusiana na uandishi wa habari za watoto yaliyofanyika leo katika  hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa shirika hilo Mussa Mgata amesema kuwa watoto ni kundi muhimu ambalo linatakiwa kuangalia kwa ukaribu zaidi, na wao kama shirika wanaangalia kwa ukaribu zaidi kundi la watoto waishio kwenye maisha magumu pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

Mgata amesema kuwa mafunzo yaliyotolewa kwa wanahabari yatasaidia sana katika kujua matatizo yanayowakumba watoto katika mazingira yao na namna ya kuyatatua, amewataka wanahabari kutumia maarifa waliyoyapata katika kusaidia kuokoa kizazi hicho.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa Shirika la Railway Children, Mary Gatama akitoa mada kuhusu watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa warsha hiyo amesema kuwa wao kama shirika watashirikiana na vyombo vya habari ambavyo huangaza jamii katika kuhakikisha changamoto zinazowakumba watoto zinapatiwa ufumbuzi.

Pia Afisa Mahusiano wa shirika hilo Henry Mazunda amesema kuwa suala la kuwalinda watoto ni jukumu la jamii nzima hivyo amewataka wanahabari kutumia kalamu zao vizuri katika kuonesha yale yanayowakumba watoto katika jamii. 


Mkurugenzi wa Shirika la Railway Children, Mussa Mgata akitolea ufafanuzi kuhusu mazingira wanayoyapitia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa warsha iliyowakutanisha waandishi wa katika mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yatakayofanyika leo katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.

Meneja Miradi wa Shirika la Railway Children, Mary Gatama akitoa mada kuhusu watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa warsha iliyowakutanisha waandishi wa katika mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yatakayofanyika leo katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mahusiano wa Shirika la Railway Children, Henry Mazunda akiwasilisha mada ya namna kuwalinda watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na namna ya kutoa elimu ya jinsi ya kuwalinda watoto hao wakati wa warsha ya iliyowakutanisha waandishi wa katika mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yatakayofanyika leo katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habariwakiwa kwenye semina ya mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto iliyoandaliwa na Shirika la Railway Children iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka Blogu ya Jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad