HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 4 February 2019

WATATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MIRUNGI

Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii.
WATU watatu wakazi wa Jijini Dar es Salaam, leo Februari 4, 2019 wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kukutwa na mirungi yenye uzito wa kilogramu 45.22.

Washtakiwa hao, Juma Hussein, Mwanaidi Mohamed na Salama Tunzamali, wamesomewa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega wa Mahakama hiyo.

Mapema,  akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Faraji Nguka amedai  katika shtaka la kwanza la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi inadaiwa, Januari 18 mwaka huu, huko  Kariakoo eneo La Mtambani Hussein na Mohamed. walisafirisha mirungi yenye uzito wa kilogramu 30.24.
Aidha mshtakiwa Tunzamali anadaiwa, siku na mahali hapo, alisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu 14.98.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kuwa ujazo wa wa dawa waliokamatwa nao Hussein na Tunzamali hauna dhamana huku mshtakiwa Mohamed akibahatika kusomewa masharti ya dhamana ambayo Pia hakuweza kuyatimiza.

 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa  hadi Februari 19, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad