HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 18 February 2019

WANARIADHA 28 KUINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MBIO ZA NYIKA NCHINI DENMARK

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la riadha Tanzania (RT) limetangaza majina ya wanariadha 28 wenye umri wa chini ya miaka 18 na zaidi kwa ajili ya kuingia kambini jijini Arusha. Vijana hao walitangazwa na  Katibu Mkuu wa RT Wilhem Gidabuday na wataingia kambini kwa ajili ya mbio za nyika  zitakazofanyika nchini Denmark mwaka huu.

Amesema mbio hizo zitahusisha wanariadha chini ya miaka 18 na zaidi ya miaka kumi na nane kwa ajili ya maandalizi rasmi ya mbio za Olimpiki zinazofanyika Tokyo nchini Japani kila mwaka. Gidabuday amesema wanariadha hao wataingia kambini  februari 20 mwaka huu ambapo wakiwa kambini watafanya mchujo utakaofikia wanariadha 20 watakaoenda katika mashindano ya mbio za nyika nchini Denmark.

Gidabuday amesema kwa mwaka huu wamekuwa na matarajio ya wanariadha wa Tanzania kupeperusha vyema bendera ya taifa katika kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini. Mshindi wa kwanza wa mbio za nyika nchini Denmark atazawadiwa kitita cha EURO elfu 60 na zawadi za medali za dhahabu na silva zitatolewa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad