HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 7, 2019

TPSF YAJADILI MAPENDEKEZO YA SERA YA KODI BAJETI YA 2019/2020

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na Wadau wake kukamilisha zoezi la kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya Kodi kuelekea Bajeti ya 2019/2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya msisitizo wa Mhe. Rais kuwa na haja ya kuangalia au kufumua upya mfumo wa Kodi pamoja na Sera yenyewe  inayoonekana kuwa mzigo mkubwa kwa Wafanyabiashara.

Simbeye amesema kazi hiyo imeanza tangu Novemba, 2018 , amesema wamekuwa wakikusanya maoni  tofauti ili kujadiliana kwa pamoja na kupata maoni hayo yatakayopelekwa Serikalini kwa ajili yakuingia kwenye maboresho ya sera ya Kodi au mfumo wa Kodi nchini.

‘’Sisi kama Sekta Binafsi tunatimiza wajibu wetu kuchangia mawazo namna gani bora ambavyo tunaweza kuweka mfumo wa Kodi ili iwe rahisi kufanya biashara Tanzania nakuweza kukuza Uwekezaji’’, amesema Simbeye.

Kwa upande wake, Mmoja wa Wanachama wa Sekta hiyo, Mwakilishi kutoka Chama cha Waajiri nchini (ATE), Dan Sora Tandasi amesema lengo lakukutana kama Wadau kutilia mkazo kwenye masuala ya Kodi, amesema Wafanyabiashara wanapata fursa kujadili changamoto zao katika Kodi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad