HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 7 February 2019

BODI YA LIGI YAWAKATALIA AFRICAN LYON KUBADILI UWANJA

Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imekataa ombi la Klabu ya African Lyon ya kuhamisha mchezo namba 271 kati yake na Simba uliopangwa kuchezwa Februari 19 mwaka huu.

Mchezo huo ulipangwa kuchezwa Arusha , African Lyon wameiandikia barua bodi ya ligi na kutaka wabadili uwanja kutoka Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kuja kucheza Uwanja wa Taifa.

Klabu ya African Lyon ya Dar iliandika barua bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) Februari 02 mwaka huu kuomba mchezo wao namba 271 dhidi ya Simba SC ufanyike uwanja wa Taifa Dar na sio Uwanja Sheikh Amri Abeid Arusha. 

Awali African  Lyon waliwaandika barua bodi ya ligi  kuomba mechi zao za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe Katika Uwanja Sheikh Amri Abeid Arusha na Bodi ya ligi kubariki maabadiliko hayo.

Katika barua yao, African Lyon imeeleza kuwa katika  mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga ambao ulifanyika mkoani Arusha walipata hasara  kutokana na gharama za kambi, usafiri na makato mbalimbali.

Imeeleza kuwa hilo ni moja ya changamoto ambapo imepelekea kuomba  mchezo wao dhidi ya Simba ambao utachezwa February 19 ufanyike katika dimba la Taifa.

Bodi ya Ligi katika barua yao waliyowajibu African Lyon wamesema kuwa ratiba hiyo haitaweza kubadilika na zaidi mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama ulivyopangwa awali na sio Uwanja wa Uhuru kama walivyoomba katika barua yao.

Simba itashuka dimbani Fevruari 19 kuvaana na African Lyon ikiwa ni siku ya tatu toka kucheza na mahasimu wao Yanga ikiwa ni mechi ya Ligi mzunguko wa pili  Februari 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad