HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 15 February 2019

TIMAYA ATAJA SABABU ZA ALI KIBA KUMSHIRIKISHA KATIKA ALBAM YAKE MPYA


Na Khadija Seif, Globu ya jamii
MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria  Enitimi Alfred a.k.a Timaya ameamua kufunguka kwa kuweka wazi sababu za kumshirikisha mkali wa Bongofleva nchini Tanzania Alikiba kwenye album yake mpya. Timaya ambaye amejijengea umaarufu kutokana na staili yake ya uimbaji, amesema kuwa ndoto yake ya muda mrefu ilikuwa ni kuhakikisha siku moja anafanya kazi na Alikiba kwani pamoja na uwezo wake mkubwa pia ni shabiki wake amekuwa akimfatilia kwa muda mrefu sana.

"Nilikutana nae kwa mara ya kwanza kwenye kazi iliyokutanisha wasanii wa nchi mbalimbali kama Amani wa Kenya,R.Kelly, Navio na wengine wengi lengo ni kuleta karibu mataifa hayo mawili Afrika na Amerika pamoja na kudumisha amani,furaha na upendo ," amesema Timaya

Hata hivyo amezungumzia katika album yake mpya iitwayo Chulo Vibes amemshirikisha Alikiba pamoja na Msanii Burnaboy kutoka Nigeria ambaye kwa sasa anafanya vizuri.

Burnaboy ni msanii ambaye anadumisha utamaduni wa kiafrika kwa ujumla na ni mfano mzuri wa kuigwa kutokana na nyimbo zake kama YE,on the low na gbona zenye mahadhi na midundo ya kiafrika zaidi na hata video zake zinahamasisha utamaduni wa kiafrika kuanzia mavazi na washiriki wa video hizo.

"Matarajio yangu ni kufanya ngoma na wasanii wa Afrika mashariki kwa nchi za Kenya,uganda na Burundi maana wasanii wa nchi hizo nao wanafanya Vizuri," amesema Timaya.

Ameongeza kuwa anataka kufanya kazi na wasanii ambao hajawahi kufanya nao kazi na ndio maana ndani ya albamu hiyo mpya ameshirikisha wasanii tofauti kabisa na kwamba anafurahia kuona muitikio umekua mzuri,hivyo basi anategemea kufika mbali zaidi kimuziki na ndio maana ndani ya albamu hiyo mpya ameshirikisha wasanii tofauti kabisa ambao hakuwahi kufanya kazi nao.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad