Mkurugenzi Mkuu wa Uniliver Tanzania David
Minja(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya
mwisho, Nsalu Mbaga(miaka 29) mkazi wa Ubungo
River side jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi
milioni moja(1,000,000/=) aliyoshinda katika
Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” iliyomalizika
mwishoni mwa wiki katika Supermarket ya Game
Mlimani City.
Mkurugenzi Mkuu wa Uniliver Tanzania David
Minja(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya
mwisho, Angel Nyange(miaka 23) mkazi wa Kimara
Mbezi jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi
milioni moja(1,000,000/=) aliyoshinda katika
Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” iliyomalizika
mwishoni mwa wiki katika Supermarket ya
Choppies Mlimani City.
WAKAZI kumi na mbili wa jijini Dar es Salaam
wafanyao manunuzi katika Supermarket za
Game,Choppies Mlimani City na Shoppers
Mikocheni,Masaki na Mbezi wamejishindia jumla ya
shilingi milioni saba na nusu(7,500 000) ikiwa ni
shilingi laki tano(500,000/=) kila mmoja katika wiki
tatu mfululizo na wiki ya nne washindi watatu
shilingi milioni moja kila mmoja.
Washindi hao walipatikana mara baada ya kununua
Omo na kuingia rasmi kwenye droo kubwa
inayochezeshwa katika Supermakert kila jumamosi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi
Mkuu wa Unilever Tanzania, David Minja kwanza
aliwapongeza washindi wote haswa watatu
waliopatikana katika droo ya mwisho kukamilisha
idadi ya washindi kumi na mbili(12) ambao ni Nsalu
Mbaga(29yr) mkazi wa Ubungo Riverside
aliyeshinda katika Supermaket ya Game Mlimani
City, Angel Nyange(23yr) mkazi wa Kimara Mbezi
alieshinda katika Supermaket ya Choppies Mlimani
City na Mueen Mohamed(59yr) aliyeshinda katika
Supermakert ya Shoppers ambao walijishindia pesa
taslimu Shilingi milioni moja kila mmoja.
Aidha David Minja aliwaomba pesa walizoshinda
wakazielekeze kwenye elimu kwa watoto wao kama
kauli mbio ya kampeni inavyo sema “Tusua Ada na
Omo”.
Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Omo
wanatambua kama jamii ya Watanzania imetoka
katika kipindi cha Siku kuu ya Chrismass na Mwaka
mpya hivyo wakaona ni jambo jema kuungana na
wanafamilia katika kipindi hiki cha watoto kwenda
shule kuchangia kwa namna moja ama nyingine
kupitia promosheni hii.
Alisema David, katika Promosheni hii ya Tusua Ada
na Omo jumla ya Shilingi milioni (7,500 000/=)
zimetolewa kwa washindi 9 ikiwa kila mmoja
alijishindia pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=)
na washindi 3 waliopatikana katika droo ya mwisho
kila mmoja alijishindia pesa taslimu shilingi milioni
moja.
Alisema David ushiriki ulikuwa wazi kwa kila mtu
lakini ilipaswa uwe na umri zaidi ya miaka 18, na
lazima ununue Omo 1kg moja ziwe pakti mbili au
500gm pakti ziwe nne au 3.5kg pakti moja,ambapo
mshiriki alipewa kuponi na kuingizwa kwenye droo
iliyochezeshwa kila jumamosi ya juma hilo.
Asanteni kwa washiriki wote mliojitokeza kushiriki
katika kipindi chote cha Promosheni hii na
hongereni sana kwa washindi wote mliobahatika
kujishindia zawadi.
No comments:
Post a Comment