HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 February 2019

SIMBA, LIPULI NANI KUVUNJA REKODI YA KUMFUNGA MWENZAKE

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba SC kesho watashuka dimbani wakiwa ni wageni kumenyana na Wanapaluhengo Lipuli FC katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018/2019.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na shauku kubwa utapigwa katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa majira ya saa kumi za jioni huku kiingilio kikiwa  VIP kwa bei 10000, Mzunguko 5000 na Watoto kwa 2500.

Sio Simba wala Lipuli wanaitaji matokeo mazuri ya alama tatu dhidi ya mwenzake  kujiweka sehemu nzuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo msimu uliopita 2017-18 hakuna timu iliyomfunga mwenzake baada ya timu zote kushindwa kufungana kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika Mchezo wa nyumbani na ugenini, Msimu huu 2018-19 wameendeleza rekodi ya kutofungana kwa kutoka 0-0 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Simba walipowakaribisha Lipuli FC.

Katika Msimamo wa Ligi Kuu Simba ikiwa nafasi ya 3 ikiwa na alama 45 na michezo 18, Yanga wao wakiwa Vinara wa Ligi hiyo wakiwa na alama 61 michezo 25, wakifuatiwa na Azam FC wenye alama 50 akiwa ameshacheza  michezo 25 pia, Lipuli FC ambao wanakibarua kizito cha kufuana na Simba kesho wao wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 38 na michezo 27.

Nani atavunja mwiko Simba au Lipuli kwa kumfunga mwenzake mara hii?ukizingatia Wekundu hao wa Msimbazi wapo kwenye kasi na Safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Emmanuel Okwi pamoja na  Middie Kagere ambaye amekuwa hatari zaidi kwa kufumania nyavu za wapinzani.

Huku Wanapaluhengo wakionekana kupoteza mchezo  wake wa mwisho aliocheza Stand United ambapo alikula kichapo cha bao 3-2 akiwa ugenini,

Simba SC wao waliendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri baada ya kumfunga Yanga hivyo kupata morali zaidi ya kuendelea kufanya vema ambapo pia katika michezo wake wa mwisho uliopigwa februari 22 Mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam alishinda bao 3-1 dhidi ya wana lamba lamba  wa Chamazi Azam FC.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad