HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 February 2019

SERIKALI KUANZISHA MACHINJIO YA KUKU

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 
SERIKALI  imesema iko kwenye mikakati ya kisera ya kuanzisha sera ya kuwepo kwa machinjio ya kisasa ya ndege wafugwao hasa katika miji  mikubwa ili kuboresha sekta hiyo. 

Hayo yameelezwa leo na Mtafiti Mkuu wa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. John Kaijage katika warsha ya siku moja ya kuangalia changamoto zinazoipata sekta ndogo ya ndege wafugwao iliyoandaliwa na taasisi inayotoa mikopo kwa Wajasiriliamali ya Victoria Finance iliyowakutanisha Wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya mnyororo wa thamani kwenye ufugaji. 

Amesema kuwa, sekta ya ufugaji wa kuku inakua kwa kasi sana, sasa hivi kuna vituo vya kutotolesha vifaranga ,huku uzalishaji wa vifaranga ukiwa umeongezeka kwa kasi kubwa

"Katika harakati za kuboresha sekta hii,  serikali inataraji kuanzisha machinjio ya kuku na kila mtu anayefanya biashara za kuku akitaka kuchinja basi atalazimika kwenda kwenye machinjio na siyo kuchinjia nyumbani labda tu Kama mtu anachinja kale ka kula nyumbani Kwake". Amesema Dkt. Kaijage. 

Dkt Kaijage Amesema, lengo la Taifa kwa sasa hi kuzalisha Tani Za  nyama kwa wingi na mayai kuanzia BIL. 3 hadi BIL. 3.4 hadi ifikapo mwaka 2020.21.22.

Aidha ameongeza kuwa, lengo kubwa la kufanya hayo yote ni kuongeza ubora wa wanyama wafugwao ili kuweza kuyapeleka mazao hayo nje ya nchi, amesema Serikali pia inatarajia kuanzisha sheria nyingi ikiwemo  kuboresha kanuni za kuzuia magonjwa kwa mtu yeyote anayeanzisha shamba La kuzalisha kuku wazazi na vituo vya kutotoresha vifaranga na mawakala lazima wasajiliwe. 

Ameongeza kuwa, mikakati iliyopo sasa hivi ni kutengeneza chanjo za kideli ambapo kuanzia mwakani kuku wote wataanza kuchanjwa  na wameiomba Serikali ipunguze bei ya chanjo hiyo ili kutokomeza ugonjwa huo kabisa. 

"Pia tunafanya tafiti  ya kubaini kuku wanaoweza kumudu mazingira ya nchi yetu kwa vijijini na mijini na pia kuweza kusaidia au kuimarisha teknolojia ya kuwabaini kuku wetu wa asili ili tuweze kubaini kuku bora na baadae kutengeneza Kuku chotara," amesema.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Victoria Finance, Julius Mcharo amesema lengo la kukutana na Wadau hao ni kuzungumzia fursa na Changamoto mbalimbali za upatikanaji wa Mikopo, Mitaji katika kuendeleza Biashara ya ufugaji kuku.
Amesema sekta hiyo imekuwa ikikimbiwa sana na  watoaji mikopo, lakini wao Kama Taasisi ya kusaidia wafanyabiashara ndogo ndogo wameona umuhimu wa kusaidia hilo ili kuwakomboa wadau wa sekta hiyo katika nyonya mbali mbali kuanzia vifaa,  mitaji na mahitaji mengine mengi. 

 Amesema kuwa uzalishaji wa Kuku ni mkubwa Katika mkoa wa Dar es salaam huku Changamoto kubwa inayoikumba sekta hiyo ni  kwamba sekta hiyo ni  kukimbiwa sana na watoaji wa mikopo licha ya kuwepo kwa  uitikio  mkubwa. 

Amesema kuwa,  "naamini yale ambayo yatazungumzwa hapa yatasaidia sana kuendeleza. Tunataka kuwasaidia hawa wafugaji kwa kuwa  mazingira ya  ufugaji yanaridhika na Mkopo huu hautakuwa wa kutoa hela halafu zikaenda kutumika ndivyo sivyo, sasa hivi tutaangalia mahitaji ya mtu kutokana na mradi wake"
Ameongeza.

 Pia amesema kuwa wataalamu wa mifugo kwa kushirikiana na wakulima au wafugaji pamoja na wale watoa huduma watakuwa wakitembelea miradi hiyo ili kujua mahitaji na maendeleo yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Victoria Finance, Julius Mcharo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua warsha ya siku moja na wadau wa sekta ndogo ya wanyama wafugwao. Amesema dhumuni kubwa la Wash hiyo ni fursa na Changamoto mbalimbali za upatikanaji wa Mikopo, Mitaji katika kuendeleza Biashara ya ufugaji kuku inayotolewa na Victoria MicrofinaceNo comments:

Post a comment

Post Bottom Ad