HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 1, 2019

RC SHINYANGA AWAONYA BODABODA WANAOLAGHAI WATOTO WA KIKE

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewaonya waendesha pikipiki, maarufu kama Bodaboda wenye tabia ya kuwapakia wanafunzi hasa wa kike na kuwalaghai matokeo yake kuwapa mimba za utotoni.
Telack ametoa onyo hilo mapema leo tarehe 31 Januari, 2019, wakati akitoa hotuba ya kufunga mradi wa “DREAMS – Innovation Challenge, keeping girls in Secondary schools” uliokuwa unatekelezwa na shirika la “amref health Africa” kwa miaka miwili katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Wilaya ya Kahama.
“Suala la bodaboda tumeshalisema sana, itabidi kukaa vikao na viongozi wa bodaboda, vijiwe vya boda boda vilivyopo karibu na shule viondolewe, watafute wateja siyo wanafunzi” amesema Telack.
Akisisitiza jambo hilo Telack amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha bodaboda wenye tabia ya kuwapatia “lift” wanafunzi wa kike waache mara moja na wakibainika wakamatwe.
Aidha, amewahimiza wanafunzi watembee kwenda shule badala ya mazoea ya kupanda bodaboda ili kuwaepusha na vishawishi visivyo vya lazima.
Amesema, mtoto wa kike ni rasilimali, hivyo wakiachwa bila uangalizi ni kuharibu Taifa la baadaye matokeo yake hata familia zao hazitadumu kutokana na kuanza ngono mapema. 
Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa pia ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kuendeleza mazuri yaliyofanywa na mradi wa DREAMS ili kuwasaidia wanafunzi hasa wa kike, kwani uelewa wa afya ya uzazi umewasaidia sana kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa vijana kutoka asilimia 2.5 mwaka 2016 hadi 0.8 mwaka 2018. 
Mradi wa DREAMS uliowafikia wanafunzi katika shule 15 ndani ya  Halmashauri ya wilaya ya Msalala, umepunguza tatizo la watoto wa kike walioacha shule kwa sababu ya mimba kutoka wanafunzi 79 mwaka 2016 hadi wanafunzi 38 mwaka 2018.
Wadau wa watoe elimu kuwazuia vijana kufanya ngono, siyo matumizi ya kondomu
Wadau wa masuala ya afya na uzazi wamesisitizwa kutoa elimu zaidi ya kuwataka vijana kuacha ngono badala ya kuwasisitiza kutumia kondomu.
Akizungumza na washiriki wa warsha ya kufunga mradi wa “DREAMS’ uliotekelezwa na 
Muda wao bado, watachoma sindano hizo hadi watakuwa tasa.
Walimu wasaidie sana watoto waweze kuishi maisha ya Kiafrika.
Hata dini zinakataza. 
Watumishi wa Hospitali pia wakiona watoto hao wanakwenda kutafuta kinga wawaulize ili wanaume wanaowarubuni wakamatwe.
Suala la kutumia vizuizi si salama sana, watoto wadogo waachane na ngono utotoni “ wanakimbilia wapi” tunapotoa njia hizi tukaona wanazikimbilia tunakuwa tunafungua milango ya zinaa, haiwezekani”
Matokeo yake hatuwezi kupunguza maambukizi ya VVU. Walimu waseme na watoto wa kike waache kujiingiza kwenye vishawishi.
 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba ya hotuba ya kufunga mradi wa “DREAMS – Innovation Challenge, keeping girls in Secondary schools” uliokuwa unatekelezwa na shirika la “amref health Africa” kwa miaka miwili katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Wilaya ya Kahama.
  Meneja mradi wa DREAMS Bw. Gasper Misungwi, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
 Dkt. Aisa Muya, Mkuu wa Miradi wa amref akitoa neno katika kufunga mradi wa DREAMS ambapo ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha mradi.
Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki katika utekelezaji wa mradi wa DREAMS kutoka amref, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad