HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 February 2019

NMB KUWAPELEKA WATEJA WAKE 6 KUJIVINJARI DUBAI


  BENKI ya NMB imewatangaza wateja watatu ambao wameibuka washindi katika droo ya mwisho ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' maarufu kwa jina la 'MastaBata'.

Wateja hao watatu katika shindano hilo, EINSTEIN STEPHEN MAGEBO, SIMON CHACHA, pamoja na NUIS PAUL KASAMBALA wakiwa na wenza wao wanatarajia kusafirishwa na Benki ya NMB kwenda nchini Dubai kula Bata kwa siku nne mfululisho safari iliyogharamiwa na NMB kila kitu.

Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya Shindano la MastaBata lililoendeshwa kuhamasisha matumizi ya mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' kwa wateja wao.

Aliongeza kuwa mbali na washindi hao wateja kibao wa NMB waliotumia mfumo huo wa malipo pia wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine wengi kujishindia simu janja za kisasa aina ya 'Samsung S9+'.

Mtangazaji kutoka kituo cha EFM, Emmanuel Kapanga (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa na Benki ya NMB ambaye amejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. Kulia ni Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed akisimamia droo hiyo. Kushoto ni Bi. Saumu Rajabu kutoka Selcom. 

Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata'. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir pamoja na Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi NMB, Bw. Manfredy Kayala  (kushoto) wakifuatilia tukio hilo. 


Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata'. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir akifuatilia tukio hilo.
Watangazaji wa kituo cha EFM radio na TV, Emmanuel Kapanga (katikati) na Tunu Hussein (kushoto waliokaa), wakizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa na Benki ya NMB ambaye amejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. Kulia ni Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed akisimamia droo hiyo.
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakishuhudia kutangazwa kwa washindi watatu wa droo ya mwisho ya shindano la MastaBata. Washindi wa mejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad