HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 February 2019

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA NBC ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR

Na ASP. Lucas Mboje, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi leo amekutana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuangalia njia bora zaidi za kudumisha na kuboresha uhusiano baina ya pande zote mbili.

Akizungumza katika mkutano huo ambao pia ulijumuisha maafisa waandamizi kutoka Benki ya NBC na Jeshi la Magereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alilishukuru Jeshi hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa Benki kupitia mikopo, akaunti za mishahara za askari pamoja na Shirika Magereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitoa huduma kwa askari wa Jeshi hilo.

“Nichukue fursa hii kulishukuru Jeshi la Magereza kwa mahusiano ya kibiashara ambayo limekuwa likitupatia, nilipongeze Shirika la Magereza kwa kuendelea kuwa mdau muhimu katika huduma zetu za kibenki pamoja na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza”. Alisema Mkurugenzi Sabi.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kwa kutembelea Jeshi hilo na kuipongeza Benki ya NBC kwa maboresho mbalimbali katika huduma zake za kibenki.

Jenerali Kasike amesema kuwa Jeshi la Magereza litaendelea kushirikiana na Benki ya NBC katika miradi yake ya kiuwekezaji na huduma mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa Jeshi hilo.

“Nikuombe Mkurugenzi Sabi na uongozi mzima wa Benki ya NBC kuona uwezekano wa kusaidiana katika huduma mbalimbali za kijamii magerezani kwani Jeshi la Magereza ni watoa huduma kwa jamii hususani huduma ya urekebishaji wa wahalifu ambao ni zao la jamii yenyewe”. Alisema Jenerali Kasike.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(kushoto) alipotembelea ofinisi za Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es salaam, leo Februari 25, 2019.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza katika kikao na uongozi wa Benki ya NBC, uliomtembelea ofinisi kwake, Makao Makuu ya Magereza jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(kushoto) akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Phaustine Kasike alipokutananaye kwa mazungumzo juu ya kuangalia njia bora za kudumisha uhusiano baina ya Benki ya NBC na Jeshi la Magereza nchini, katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019. Wengine kulia ni Maafisa Waandamizi wa Bendi hiyo.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) pamoja na Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Mhandisi, Tusekile Mwaisabila9kushoto) wakifuatilia mazungumzo hayo katika Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi(wa tatu toka kushoto) pamoja na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza na Benki ya NBC katika Makao Makuu wa Magereza, jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019(Picha na Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad