HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 16, 2019

DKT. MPANGO ATETA NA WAFANYAKAZI NA KUHIMIZA MAADIDLI NA UWAJIBIKAJI KAZINI

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo na kuzungumza nao namna bora ya utekelezaji wa  majukumu ya Wizara ili kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

 Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema Wizara ya  Fedha na Mipango ni kitovu cha Serikali hivyo  Watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na  taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija.

Amesema kila mtumishi anawajibu wa kufanya kazi kwa weledi, bidii na kushirikiana na kila mmoja katika nafasi yake ili kuboresha utendaji kazi na kukuza uhusiano mahala pa kazi.

Aidha Waziri Mpango aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, Uchambuzi wa Sera za Taifa na uanzishwaji wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki-GePG.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu amemhakikishia Waziri Mpango kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa ukamilifu ili kuboresha utendaji kazi wa Wizara hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), katika kikao na Watumishi hao Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akifafanua jambo wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), Jijini Dodoma.
 Mjumbe wa TUGHE Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mariam Kihange, akichangia mada wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Gisela  Mugumira akifafanua jambo wakati wa  kikao na  Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma, kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw.  Alfred Dede.
 Mwakilishi wa Kamishna wa Bajeti Bw. Sigsbert Kavishe akichangia hoja katika wa  kikao na  Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango,  kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu, kulia ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Victus Tesha  Jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad