HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 4 January 2019

ZFA YATANGAZA MAPUMZIKO YA LIGI KWA MWEZI MZIMA


Na Ripota Wetu, Zanzibar
Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetangaza mapumziko ya ligi kupisha mashindano ya Mapinduzi Cup ili yachezwe kwa ufanisi zaidi.

Mapumziko hayo ni ya mwezi mzima kuazia 01/01/2019 hadi 05/02/2019 wakati huo wa mapumziko pia ZFA utautumia muda huo kwa mujibu wa kalenda kufanya uhamisho na usajili wa dirisha dogo kuazia 01/01/2019 hadi 25/01/2019 baada ya hapo zfa itaendelea na utaratibu wa kuhakiki na kupitisha uhamisho, usajili na kutoa block ya usajili wa dirisha dogo.

Ligi Kuu Zanzibar inakwenda mapumziko huku timu zote zikiwa zimecheza nusu ya mechi zao yaani kila timu imecheza mechi kumi na nane (18) ligi hiyo inaongwa na KVZ kwa kujikusanyia point arubaini na tatu (43)

Ligi daraja la kwanza Kanda inakwenda mapumziko huku timu zote zikiwa zimecheza mechi kumi na tatu (13) na kwa upande wa ligi ya daraja la pili Taifa ambayo inachezwa kwa mfumo wa makundi makundi yote matatu timu zote zimecheza nusu ya michezo yao na baada ya kumaliza mapumziko watarudi viwanjani kwa michezo ya marudiano

Mapumziko hayo ni yale ambayo yameandikwa kwenye kalenda ya ZFA ya 2018/2019 haijabadilishwa na ZFA haina mpango wa kupunguza wala kuongeza siku katika usajili huo wa dirisha dogo kila timu inatakiwa kufuata kalenda ili kuondoa usumbufu.Mapumziko hayo ya ligi yataishia 05/02/2019 kutoka hapo timu zitarudi viwanjani kwa kuaza rasmi na michezo ya FA CUP ambayo itachezwa kwa kushirikisha timu zote za daraja la pili taifa na timu ishirini na nne (24) za daraja la kwanza kanda ya Pemba na Unguja.

Timu kumi na tisa (19) za ligi kuu na timu nane (8) daraja la kwanza Kanda zitabaki kusubiri hatua ya pili ya mashindano hayo ya FA CUP

Ikumbukwe kwa mujibu wa kanuni bingwa wa Mashindano ya FA CUP atakuwa muakilishi wa nchi kwa mashindano ya kombe la shirikisho barani Africa Mashindano hayo ya FA CUP yatachezwa kwa mfumo wa mtoano na yataaza kwa timu za Pemba kucheza kwao na timu za Unguja kucheza kwao timu zitaungana hatua ya robo fainal Pemba timu nne (4) na timu Unguja nne (4)

ZFA inawatakia mapumziko mema ya dirisha dogo familia yote ya mpira wa miguu huku ikiwasisitiza viongozi wa vilabu kufanya uhamisho usajili kwa wakati na mambo yote yanayo husu fedha iwe kununuwa fomu za usajili uhamisho au kulipia wachezaji malipo yafanywe kwa njia ya bank kupitia account ya ZFA TAIFA PBZ 0406097000 vifaa vyote vinavyo hitajika kwa ajili ya usajili uhamisho wa dirisha dogo vipo ofisini vya kutosha.


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad