HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 6 January 2019

WAZIRI HASUNGA AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea).

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa  Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Muonekano wa hatua zilizofikiwa za mradi wa ujenzi wa  Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka umaojengwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akisalimiana na Mwenyeji wake ambaye ni Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma Ndg Nicodemus Massao wakati alipowasili kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo nunua mazao ya wakulima nchini.

Wakati NFRA imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.

Alisema kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haitalifumbia macho kamwe.

Pamoja na mambo mengine waziri Hasunga ameupongeza Uongozi wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kwa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) katika maeneo nane ya kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Mradi huo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi umeanza kujengwa katika Manispaa ya Songea (Ruvuma), Dodoma, Mpanda (Katavi), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara) ambapo Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

Mhe Hasunga amesema kuwa pundi utakapokamilika ujenzi wa maghala na vihenge hivyo utapunguza gharama mbalimbali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kununua madawa ya kufukiza mahindi sambamba na gharama za kununua magunia ya kuhifadhia mahindi.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba kuweka msisitizo zaidi wa kununua nafaka ya mahindi kwani katika kipindi chake serikali haitotoa hela kwa ajili ya ununuzi wa mahindi badala yake NFRA ijipange kibiashara ili iweze kununua nafaka nyingi na kujiendesha.

Alisema kuwa huu sio muda wa NFRA kusubiri kupewa mtaji na serikali badala yake kufikiria tofauti na kuanza kufanya biashara ili kufikia walau ununuzi wa nafaka kwa Tani zaidi ya 300,000.

Vilevile, ameutaka Wakala wa majengo Tanzania (TBA) kusimamia kwa weledi mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wananchi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad