HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 17 January 2019

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA KAMPUNI YA TANZAPLUS

Waziri wa Madini, Doto Biteko tarehe 16 Januari, 2019 amekutana na kampuni  inayojishughulisha na uyeyushaji wa madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya Tanzaplus katika Ofisi za Wizara ya Madini zilizopo jijini Dodoma.  Kikao chake  pia kilishirikisha Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Mhandisi Migodi Mkuu kutoka Tume ya Madini, Conrad Mtui pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Madini. 

Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kampuni ya Tanzaplus Minerals kwa kushirikiana na kampuni nyingine ya AIMGROUP kutambulisha teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini. Waziri Biteko aliitaka kampuni ya Tanzaplus kuendelea kufanya utafiti zaidi juu ya mfumo husika kwa kushirikisha wadau mbalimbali  kabla ya kuwasilisha pendekezo lake Serikalini.
 Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akizungumza na watendaji wa kampuni inayojishughulisha na uyeyushaji wa madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya Tanzaplus. Waliokaa kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal, na Upendo Fatukubonye na Hamis Mhando ambao ni watendaji kutoka kampuni ya Tanzaplus.
 Mkurugenzi kutoka kampuni ya Tanzaplus, Hamis Mhando (kulia) akielezea  jinsi teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini inavyofanya kazi.
Wataalam kutoka Wizara ya Madini wakinukuu maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad