HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 9 January 2019

TTB KUWEZESHWA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NDANI NA NJE YA NCHI

NA LUSUNGU HELELA-DSM
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Serikali inaangalia  namna bora ya  kuiwezesha  Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB)   ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo badala ya  kila Taasisi kujikuta  ikitangaza vivutio vya Utalii ilivyonavyo kivyake . 

Ameyasema hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 wakati alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha "Jambo Tanzania" kinachoruka TBC1na kipindi cha "Asubuhi Hii" kinachoruka TBC Taifa Mikocheni  jijini Dar es Salaam

Aidha, ameitaka TTB ianze  kutangaza vivutio vya utalii kwa mfumo wa vifurushi (Packages) ili watalii wanapokuja waweze kutembelea sehemu mbalimbali za vivutio badala ya kwenda moja kwa moja Hifadhi ya Taifa ya Serengeti au Ngorongoro pekee." Tunataka mtalii kabla hajafika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha aende akaone jiwe la maajabu la Gangilonga akitoka hapo apitie Boma la Mjerumani ndo aende zake Ruaha" amesema Mhe.Kanyasu.

Pia amesema Wizara inajipanga kuanza kutumia watu maarufu wakiwemo wasanii pamoja na wacheza mpira kwa kuwadhamini lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  akifanya mahojiano kwenye kipindi cha "Jambo Tanzania" kinachoruka TBC 1 akielezea mikakati ya wizara hiyo jinzi ilivyojipanga kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii leo  Mikocheni  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtangazaji wa TBC1, Mbozi Katala
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  akifanya mahojiano kwenye kipindi cha "Asubuhi Hii " kinachoruka TBC TAIFA akielezea mikakati ya wizara hiyo jinzi ilivyojipanga kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii leo  Mikocheni  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtangazaji wa TBC TAIFA, Asha Haji 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad