HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 9, 2019

TAASISI YA WAJIBU YATOA MAONI SAKATA LA SPIKA WA BUNGE NA CAG

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

TAASISI ya WAJIBU inayojihusisha na masuala ya uwajibikaji hapa nchini imetoa maoni yake kuhusiana na tamko la Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad juu ya kauli aliyoitoa kwenye mahojiano na kituo cha redio cha idhaa ya Kiswahili ya Redio ya umoja wa Mataifa (UN Redio)

Kupitia taarifa yao waliyoitoa kwa vyombo vya habari WAJIBU wameeleza kuwa wakiwa miongoni mwa taasisi fikra za uwajibikaji nchini wameona ni vyema itoe maoni huru kwa kuzingatia maslai mapana katika uwajibikaji na utawala bora nchini kwa kuzingatia kuwa Bunge na CAG ni vyombo vinavyotambuliwa kikatiba.

Katika maoni yao WAJIBU wamesema kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa taasisi hizo mbili katika kusimamia rasilimali za Umma na kukuza uwajibikaji na utawala bora ni vyema busara ya hali ya juu ikatumika baina ya pande hizo mbili. Na kueleza kuwa dhana za uwajibikaji na utawala bora nchini vitaimarika iwapo tu kutakuwepo na uhusiano na mzuri kati ya taasisi zote za uwajibikaji na usimamizi nchini.

Aidha wameeleza kuwa taasisi hizo mbili zina umuhimu mkubwa hivyo zinatakiwa kushirikiana kwa karibu sana katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora nchini na wameshauri wananchi kutoa maoni yatakayoboresha na kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo.

WAJIBU wamesisitiza kutumika kwa busara za hali ya juu bila kuathiri uhuru wa kikatiba uliotolewa kwa mhimili Bunge na kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad