HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 21, 2019

NMB YATOA MFUNGAJI BORA BBL 2018/19



Mfungaji Bora wa mashindano ya kikapu kwa taasisi za fedha (BBL 2018/19), Kaikai Leka wa NMB, akipokea kombe dogo kama zawadi ya ufungaji bora kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori, baada ya pambano la fainali ya michuano hiyo Januari 19 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akipaa hewani kuifungia timu ya kikapu ya NMB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.

Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akipaa hewani kuifungia timu ya kikapu ya NMB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa leo Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Juma Kimori, akimkabidhi nahodha wa timu ya kikapu ya NMB, Danford Kisinda, kombe la ushindi wa pili wa Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya DTB, iliyopigwa leo Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda kwa pointi 90-73.



NA MWANDISHI WETU


NYOTA wa mpira wa kikapu wa kikosi cha Benki ya NMB, Kaikai Leka, ameibuka Mfungaji Bora (Best Scorer) wa Ligi ya Kikapu kwa Taasisi za Fedha (Bankers Basketball League - BBL 2018/19), baada ya kufunga pointi 160 katika mechi za michuano hiyo iliyofikia tamati juzi, jijini Dar es Salaam.

Katika fainali ya kukata na shoka jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, Benki ya DTB iliibuka mshindi baada ya kuifunga NMB kwa pointi 90-73, huku mchezaji wa NMB Leka akifunga zaidi ya nusu ya pointi zao hivyo kutangazwa Mfungaji Bora akifuatiwa na Acram Majid wa DTB, aliyefunga pointi 129.

Leka alizawadiwa Tuzo ya Mfungaji Bora, kama ilivyokuwa kwa Mchezaji Bora (MVP) Leonard Benedict wa DTB, Beki Bora Frank Mwemezi wa DTB na kinara wa kufunga pointi tatu kwa mtupo mmoja (Leading Three Pointer), Acram Majid aliyefanya hivyo mara 13 katika michuano yote.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi na kufunga mashindano, Mratibu wa BBL 2018/19, Gozbert Boniface, alizipongeza timu sita zilizoshiriki michuano hiyo kwa upande wa mpira wa kikapu na kuzitaka kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao, utakaoanza baadaye mwaka huu.

“Tunaipongeza DTB kwa kutwaa taji, lakini pia kwa NMB kwa kutwaa medali za fedha za ushindi wa pili na pia kwa kutoa Mfungaji Bora wa michuano hii, iliyoshirikisha mabenki sita ya NMB, DTB, Azania, CRDB, TADB na NBC,” alisema Boniface wakati akitoa neno la shukrani.

Kwa upende wake, Mgeni Rasmi wa fainali hiyo, Juma Kimori, ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, aliwapongeza waratibu kwa wazo zuri la kuanzisha michuano hiyo, iliyoimarisha mahusiano baina ya taasisi za kifedha nchini, huku akiwapongeza mabingwa na washindi wa pili wa michuano hiyo.


Mshambuliaji wa NMB, Kaikai Leka, akiwatoka walinzi wa timu ya kikapu ya DTB wakati wa fainali ya Michuano ya Mabeki (BBL 2018/19), dhidi ya timu hizo mbili uliyopigwa Januari 19 kwenye Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam. DTB ilishinda pointi 90-73.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad