HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 28 January 2019

NMB YAKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA SH.MILLIONI 15/- KWA SHULE 5 ZA MSINGI, WILAYA YA TEMEKE

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Joel Mwakabibi akiwa na Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd kwa pamoja wakimuonyesha Kompyuta mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini .
Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akiwa na Watumishi wengine wa Benki ya NMB wakipokea Cheti cha Shukrani kutoka Shule ya Msingi Mabatini.
Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akikabidhi Bati kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Joel Mwakabibi ikiwa ni azma ya Benki hiyo utoa asilimia Moja ya faida.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Benki ya NMB imetoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 15/- kwa Shule 5 za Msingi katika Manispaa ya Temeke ikiwa ni katika azma yake ya utekelezaji wa utoaji huduma zake kwa jamii.

Benki hiyo imetoa msaada wa Madawati 51, Kompyuta 5 na Mabati 200 huku  ikiahidi kuendelea na utoaji wa msaada huo kwa jamii kama inavyofanya kwenye Nyanja ya Afya, na Majanga.

Akizungumza baada yakukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki hiyo, Kanda ya Dar es Salaam na Zanziabr, Badru Idd amesema kuwa wamefanya kwa mtazamo kwa kulijenga Taifa, amesema wanachukua asilimia moja kuhakikisha wanaisaidia jamii.

Badru amesema kuwa asilimia hiyo ya faida inayotokana kila mwaka wanaigawa kuisaidia jamii katika Nyanja za Elimu, Afya na Majanga yanayoikumba jamii husika.‘’Sasa hivi tunaenda Kiteknolojia kuhakikisha tunamsaidia Mtanzania kokote pale alipo, Matawi yetu yapo 206 na ATM 7OO’’, amesema Badru.

Baada yakupokea msaada wa vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Joel Mwakabibi amesema NMB imekuwa mfano kwa Taasisi nyingine za Kifedha, amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia Wanafunzi wengi katika Shule hizo kwa kazi nzuri inayofanywa na Taasisi hiyo.

Mwakabibi amesema kuwa jitihada za NMB katika kusaidia Watoto inaweza kugusa maisha ya wazazi hivyo kuwafungulia Akaunti watoto hao, wenye ndoto zakuwa tegemeo la Taifa la kesho.‘’Manispaa ya Temeke ina uhitaji wa Vifaa vingi kwa ajili ya wingi wa Wanafunzi, tunawashukuru NMB na tunaomba Taasisi nyingine kuiga mfano kwa Taasisi hii’’, amehoji Mwakabibi.

NMB imetoa msaada huo wa Mabati 200, Kompyuta 5 na Madawati 51, ikiwa na utekelezaji wa azma yake ya utoaji msaada kwa jamii ikiwa ni kutoa asilimia Moja ya faida inayopatikana kila mwaka.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad