HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 3, 2019

MTANZANIA ATAMBA KATIKA KICK BOXING NCHINI CHINA, AMTWANGA MCHINA KWA KNOCK OUT

Na Sultani Kipingo
Mwanafunzi Mtanzania anayesoma nchini China Isaack Ibrahim Emmanuel juzi ameibuka kidedea katika mchezo wa kick boxing baada ya kumpiga kwa KO Mchina Zi xiǎo yún yǔ katika Mjini Jillin.

Isaack, ambaye anasomea uhandisi wa Madawa (Pharmaceuticals engineering) katika Chuo Kikuu cha Liaoning jijini Shenyang, ameushangaza umati mkubwa wa Wachina baada ya kucheza kwa ustadi na hatimaye kumgaragaza Zi ambaye hajawahi kupigwa hata mara moja.

Mpambano huo wa Kg 60 umempa umaarufu mkubwa Isaack kiasi kwamba hata waandaaji wa mapambano wameanza kupigana vikumbo kumtaka acheze mapambano zaidi. Akiwa na uwezo wa kutumia kwa kasi ya ajabu miguu na mikono yote, wataalamu wa mchezo huo wamemtabiria makubwa kijana huyu wa kutoka Mwanza.

Akiongea na michuzi tv kwa njia ya mtandao, Isaack amesema yuko fiti kupambana na yeyote na popote huku akiendea na Masomo bila wasi.

Isaack Ibrahim Emmanuel akimenyana na Mchina Zi xiǎo yún yǔ katika Mjini Jillin.
Isaack Ibrahim Emmanuel akimpa kibano Mchina Zi Xiǎo Yún Yǔ katika Mjini Jillin.
Isaack Ibrahim Emmanuel akitangazwa mshindi dhidi ya Mchina Zi Xiǎo Yún Yǔ katika Mjini Jillin.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad