HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 3, 2019

MAKOSA YA UBAKAJI NA KUPATIKANA NA SILAHA YALIONGEZEKA MKOANI PWANI 2018-WANKYO

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MAKOSA ya ubakaji yametajwa kuongezeka kutoka 206 kwa mwaka 2017 na kufikia 271 mwaka 2018, mkoani Pwani. Aidha kupatikana na silaha mwaka 2017 yalikuwa makosa tisa ambapo mwaka uliopita yameongezeka na kufikia 26 .

Akielezea tathmini ya hali ya uhalifu katika kipindi cha mwaka 2018 ikilinganisha na mwaka 2017 ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa alisema tathmini ya kijumla inaonyesha wamepunguza matukio 151 makubwa. Alisema, makosa ya ubakaji yameonekana kupanda kutokana na uelewa kwa jamii na mwamko wa kuripoti matukio hayo polisi. 

Wankyo alieleza, matukio ya mauaji yalikuwa 61 ikilinganisha na matukio 70 yaliyoripotiwa mwaka 2017. "Makosa ya kufanya biashara ya kusafirisha binadamu mwaka 2018, yalikuwa 03 ikilinganishwa na makosa 05 yaliyorekodiwa mwaka 2017"alifafanua Wankyo. 

Kamanda huyo alisema kuwa, makosa ya unyang 'anyi wa kutumia silaha mwaka 2017 yalikuwa 21 na mwaka 2018 makosa hayo ni 13. Unyang'anyi wa kutumia nguvu mwaka 2017 yaliriporiwa makosa 126 ,wakati mwaka 2018 makosa ya namna hiyo yameripotiwa makosa 52 .

Alisema, jeshi hilo pia limefanikiwa kudhibiti uingizaji bidhaa kupitia bandari bubu wilayani Bagamoyo kwa kukamata makosa 27,watuhumiwa 31 pamoja na madumu 5,435 ya mafuta ya kula aina mbalimbali. "Sukari kutoka nchi za nje mifuko 78, mabello 20 ya nguo za mitumba aina mbalimbali ikiwemo manne ya khanga na vyombo vya moto vilikamatwa ikiwa ni pamoja na pikipiki sita na magari matatu. "alieleza Wankyo.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad