HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 27, 2019

JITIHADA ZA GULAMALI KUWEZEKA SEKTA YA ELIMU ZAONESHA MATUNDA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2018

KATIKA utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Manonga nguvu na jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Seif Gulamali katika sekta ya elimu zimezaa matunda katika sekta ya elimu na hii ni mara baada ya kutoka kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018. Matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka jana kwa shule za Serikali ufaulu umeongezeka kwa mwaka tofauti na mwaka uliopita na hiyo ni kutokana na uboreshaji wa miundombinu pamoja na vitendea kazi katika sekta ya elimu.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa shule za Sekondari Ziba, Nkinga, Simbo, Ichama, Mwisi, Choma, Igoweko, Sungwizi, Ndembezi, Ngulumwa, Misana na Mwashiku zikifanya vizuri kwa kutoa wanafunzi zaidi ya 200 waliopata daraja la kwanza hadi tatu. Aidha shule ya ya Sekondari Ichama kutoka kata ya Chabwata imefanya vizuri kwa shule yenye wanafunzi chini ya 40 kwa kushika nafasi ya 3 Kimkoa na kushika nafasi ya 183 kati ya shule 1371 kitaifa.

Hali hiyo imetokana na juhudi za Mbunge wa jimbo hilo kwa kisimamia vyema sekta ya elimu ambapo alihaidi kusimamia na kutoa wasomi wengi Manonga, Ikumbukwe kuwa mapema Julai mwaka jana Gulamali alifungua mabweni kwa ajili ya kidato cha tano na sita  katika Sekondari ya Ziba, na kukabidhi madarasa 3  katika sekondari ya Mwisi.

Gulamali amekuwa akitoa chachu kwa vijana wanaofaulu kidato cha nne na kuendelea na kidato cha tano kwa kuwalipia ada na hadi sasa zaidi ya wanafunzi 140 wamenufaika kwa kusomeshwa na Ofisi ya Mbunge na utaratibu huo umezidi kutoa hamasa kwa wanafuzi walioko mashuleni kusoma kwa bidii ili waweze kunufaika zaidi.

Pia ikumbukwe kuwa Mbunge huyo huzunguka katika shule zote za Serikali jimboni humo na kuzungumza na walimu pamoja na wanafunzi katika kuhamasisha ufaulu kwa kuwalipia ada wanafunzi wanaochaguliwa kuingia kidato cha tano hali ambayo imekuwa ikiwahamasisha wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Vilevile ametoa pongezi kwa walimu na wanafunzi kwa kuzidi kunyanyuka zaidi kielimu katika Jimbo la Manonga na Wilaya ya Igunga na hadi kufikia mwaka 2025 hali ya elimu Jimboni humo itaimarika zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad