HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 January 2019

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 07 kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa bila kulipia ushuru.

Kuhusiana na uingizaji bidhaa nchini bila kulipa kodi Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wanne, wakiwemo, Obley Sambakusi (32) raia wa Malawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Lilongwe, Tamandani Kachimela [31] Mkazi wa Lilongwe Malawi, Imtiaz Ahmed (45) dereva na Mkazi wa Kyela, Boaz Salvatory (28) dereva na Mkazi wa Kyela.

Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 21.01.2019 majira ya saa 21:15 usiku katika Roadblock Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya wakiwa na bello hamsini (50) za vyandarua, kila bello moja likiwa na vyandarua 50 ikiwa ni jumla ya vyandarua 2500 wakiviingizwa nchini bila kulipia ushuru wakitumia gari zenye namba za usajili T.471 DDY aina ya Toyota Noah na T.301 CTX aina ya Toyota Noah kutoka nchini Malawi na kuhusiana na shtaka hilo Upelelezi unaendelea.

Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linalishikilia gari lenye namba za usajili T.867 DHK aina ya Toyota Noah likiwa limebeba mafuta ya kula aina ya MERU GOLD ndoo 45 zenye ujazo wa lita 20 na mafuta aina ya NONA PALM dumu kumi zenye ujazo wa lita 20 toka nchini Malawi. 

Gari hilo likiwa na bidhaa hizo ambazo hazijalipiwa ushuru lilikamatwa tarehe 22.01.2019 saa 06:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya baada ya dereva wake kusimamishwa na askari na kukaidi amri halali na ndipo askari walipotumia mbinu za nyingine na kufanikiwa kukamata gari hilo. Dereva wa gari hilo alikimbia na kutelekeza gari hiyo. Juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia Enele Kakisungu (31) Mkazi wa Kagwina, Grace Evance (36) Mkazi wa Uyole, na Ruth Andrew (35) Mkazi wa Kiwira Road wakiwa na mafuta ya kupikia lita 50 aina ya Kook Well toka nchini Malawi na Juice box 11 za unga aina ya Baks kwa ajili ya kutengenezea juice. Watuhumiwa walikamatwa tarehe 19.01.2019 saa 15:00 alasiri huko katika road block - Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa walikuwa wakiingiza bidhaa hizo nchini bila kulipia ushuru kwa kupitia njia za panya.
 Magari yaliyokamatwa kwenye matukio mawili tofauti yakiwa na bidhaa zilizokwepa ushuru
 Meneja wa Forodha Mikoa ya Mbeya na Songwe Johnmasa Michael akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuhusiana na uingizaji bidhaa nchini bila kulipa kodi 
 Ndoo za mafuta ya kupikia na vyandarua vilivyokamatwa kwa kukwepa kulipia ushuru wa forodha.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad