HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 9 January 2019

IDADI YA WAGONJWA WA FISTULA YAPUNGUA KWA KASI ARUSHA


NA VERO IGNATUS-ARUSHA.

Kutokana na wingi wa wakinamama wenye tatizo la ugonjwa wa fistula kuendelea kujitokeza na kupata matibabu katika kituo maalumu cha Kivulini Maternity Center kilichopo wilayani Arumeru mkoani Arusha,imeelezwa kuwa kwasasa idadi ya wagonjwa wa tatizo hilo imepungua kwa kiasi kikubwa mkoani humo


Akieleza ukubwa wa tatizo hilo daktari Francis Mollel ambae ni mtaalamu wa magonjwa wakina mama anasema kuwa kutokana na elimu ya masuala ya afya ya uzazi kumesaidia kupunguza idadi ya wagojwa wa fistula kwani husababishwa na uzazi pingamizi. 


Namba ya wagonjwa inaendelea kupungua kutokana na  elimu ya afya imekuwa ikitolewa mara kwa mara, uelewa ni mkubwa kwa wagonjwa kwenda hospitali mapema kujifungua kwani tatizo hili la fistula linatokana na uzazi pingamizi. ''Alisema Dkt Mollel


Dkt. Mollel amesema kuwa wagonjwa wa mwisho waliofanyiwa upasuaji walikuwa 23, na hivi karibuni wanatarajia upasuaji mwingine kufanyika machi 2019  idadi itaongezeka zaidi kwani wanatazamia kuingia kwenye  kambi za wakimbizi pia 

Katika hatua nyengine mtaalamu huyo amebainisha namna wanavyo wanawafikia na kuwahudumia wagonjwa wanaoishi na tatizo la fistula hususani katika maeneo ya vijijini ambapo amesema  kambi ya fistula  wanaifanya kila baada ya miezi mitatu. 


Mara nyingi tunawatuma wataalamu wetu kwenda kuwatafuta wagonjwa huko nje, ambapo wakishapimwa na kugundulika kuwa wana fistula yenyewe, tunawalaza, tunawafanyia upasuaji, mgonjwa anakaa hospitalini siku 14 na tunamuangalia kama hana tatizo tena tunamruhusu kurudi nyumbani akiwa ameshapona kabisa. '' Alisema Dkt. 


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho gambo ambae ametembelea kituo hicho kwa lengo la kufahamu maendeleo na changamoto za utioaji huduma kwa wagonjwa akatumia fursa hiyo kuahidi kufanyia changamoto zilizo katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na changamoto ya hitaji la damu salama pamoja na barabara kufika eneo la kituo. 

''Changamoto kubwa ya waliyonayo chanjo, damu salama na wametuomba kama mkoa kuwasaidia, pia wana changamoto ya barabara hivyo tumezungunza na Tarura kama wanaweza kutengeneza barabara ya kilometa 1.2''Alisema Gambo

Mratibu wa TARURA Mhandisi Edward Amboka akiahidi kuanza kufanya tafiti kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo mara moja. 

Kituo hicho ni maalumu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa mbalimbali wenye tatizo la Fistula na uzazi hususani wagojwa walio masikini bila gharama yoyote.
Dkt. Francis Mollel ambae ni Mtaalamu wa Magonjwa ya wakina mama. Picha na Vero Ignatus. 


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad