HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 31 January 2019

CHUO CHA BANDARI KUFUNDISHA KISASA ZAIDI, MTAMBO WA KUFUNDISHIA WANUNULIWA

Chuo cha Bandari ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kimejipanga kupokea mitambo ya kisasa ya kufundishia ili kukifanya kiwe cha kisasa zaidi. Kwa kuanzia, TPA imeshaingia mkabata wa kununua mtambo mkubwa wa kufundishia uendeshaji wa vyombo vyote vya kupakia na kupakua mizigo bandarini yaani ‘full Mission Crane Training Simulator’.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo hicho, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kwamba mtambo huo, unaotarajiwa kugharimu takribani Shs.1.5bn ni wa kisasa na wenye manufaa makubwa zaidi kwa Chuo.
“Mtambo huu utafungwa ndani ya miezi sita kuanzia sasa na kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka ujao wa fedha,” amesema Mhandisi Kakoko.

Mhandisi Kakoko ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, amesema kwamba Mamlaka itaendelea kuwekeza katika vifaa ili kukifanya Chuo hicho kiwe cha kisasa zaidi. Aidha, Chuo kimezindua tovuti pamoja na mfumo wa TEHAMA ‘Students Information Management System’ amesema Mhandisi Kakoko na kuongeza kwamba juhudi hizi zinalenga kuimarisha na kusimamia ubora wa huduma zitolewazo na Chuo.

Kwa upande, Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Joseph Kakeneno amesema kwamba Chuo kinakusudia kutoa Stashahada za juu na Shahada ya kwanza ya kuongeza ujuzi wa utendaji kazi ‘Competence Based’. Dkt. Kakeneno amesema kwamba shahada hizo wanazotarajia kuzianzisha katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, ni katika taaluma zinazohusiana na huduma za meli, maji na menejimenti ya shughuli za bandari. Amesema kwamba kwasasa Chuo kina karakana nne (4) za mafunzo kwa vitendo, moja kwa kila fani ya ‘Mechanical, Civil, Automotive, Eletrical na mabara moja ya kompyuta na maktaba moja.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko akihutubia wageni wakati wa mhafali ya Chuo cha Bandari
 Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa zawadi Waziriwa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwelwe, C, Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, R, na Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt Joseph Kakeneno.
 Wanafunzi waliomaliza masomo yao wakiwa katika mahaafali hayo

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad