HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 20, 2019

Bilioni 3.5 kujenga makazi ya Askari Dodoma

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akitoa maelezo ya Ujenzi wa Nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu akimuuliza maswali Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea eneo la Medeli, jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Medeli,jijini Dodoma zinapojengwa nyumba mia moja(pichani) kwa ajili ya makazi ya askari polisi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akiwaongoza  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama walipotembelea eneo la Ihumwa ,jijini Dodoma yanapojengwa Makao Makuu ya wizara hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Baadhi ya nyumba  zinazojengwa katika eneo la Medeli ikiwa ni mkakati maalumu wa Serikali ya Awamu ya Tano kujenga makazi ya askari polisi nchi nzima ili kuwaondolea askari changamoto za makazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Jumla ya nyumba Mia Moja za Makazi ya Askari zimeanza kujengwa  mkoani Dodoma  ikiwa ni Mpango  wa  serikali  kukabiliana na changamoto za makazi ya  Askari Polisi watakaohamia hivi karibuni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza agizo la kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani hapa

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama kutembelea eneo la Medeli Mashariki ambapo Awamu ya Kwanza ya mradi huo ukihusisha nyumba 30, Ujenzi wa Shule ya Awali, Ujenzi wa Kantini, Ujenzi wa Viwanja vya Michezo tayari imeshaanza

“Ujenzi wa nyumba hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa nyumba kama hizi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha askari wanaishi sehemu safi na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha ujenzi wa nyumba kama hizi  kote nchini unafanyika kwa gharama nyepesi na tukitumia wataalamu wa ujenzi waliopo serikalini na katika Jeshi la Polisi..” alisema Masauni

“…..mradi huu utakua na awamu tatu ambapo mwezi April mwaka jana, awamu ya kwanza ilianza na kutarajiwa kukamilika April mwaka huu huku awamu zilizobakia zikitarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu na  hadi kufikia mwaka kesho katikati awamu zote zitakua zimekamilika” aliongeza Masauni

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Mussa Zungu amewapongeza Viongozi wa wizara na Jeshi la Polisi kwa mradi huo huku akishauri miradi mingine wajenge maghorofa ili kuweza kuitumia ardhi waipatayo kwa matumizi mengine sambamba na ujenzi wa makazi ya askari.

“Nawapongeza kwa kutumia mapato yenu wenyewe ya ndani kuanzisha miradi mikubwa kama hii na sisi wajumbe wa kamati tumeridhishwa na hatua hizi za kukabiliana na makazi ya wapiganaji wetu wanaotulinda usiku na mchana na nchi yetu kuendelea kuwa na amani,” alisema Zungu

Jumla ya gharama ya mradi huo wa nyumba Mia  Moja za Makazi ya Askari Polisi ni Bilioni Mia Tatu na Laki Tano ambazo zinatokana na Mfuko wa Tuzo na Tozo ikiwemo malipo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na askari polisi na faini zinazotozwa na askari kwenye makosa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad