HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 30 January 2019

BENO KAKOLONYA AMEANDIKA BARUA YA KUVUNJA MKATABA- LUKUMAY

Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa tayari wameshamalizana na golikipa wao Beno Kakolanya ingawa wamepokea barua ya kuvunja mkataba.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo Samwel Lukumay amesema kwamba mlinda mlango Beno Kakolanya haidai klabu hiyo katika kipindi hiki baada ya kumaliziwa stahiki zake ambazo amekuwa akizidai.

Lukumay amesema ingawa wameweza kumaliza kumlipa stahiki zake zote, uongozi kwa  siku ya jana umepokea barua kutoka kwa mwanasheria wa Beno wakihitaji kuvunja mkataba wake jambo ambalo amedai uongozi utakaa na kulijadili kwa undani kwani mchezaji alishalipwa stahiki zake kabla ya madai hayo ya kuvunja mkataba.

Amesema kwamba kimsingi hadi kufikia sasa mchezaji ni wa Yanga hivyo kama dhamira yake ni kuvunja mkataba basi ni vizur taratibu zikafuatwa.

Aidha amesema kwamba swala la yeye na kocha mkuu wa klabu Mwinyi Zahera ni jambo ambalo mchezaji alipaswa kuwasiliana na uongozi au kocha mwenyewe ili kulipatia ufumbuzi jambo ambalo hakulifanya.

Kwa mujibu wa Lukumay amesema kwamba katika usajili wa msimu uliopita Beno amesaini mkataba wa miaka miwili hivyo bado angali na mkataba wa muda mrefu kusalia ndani ya klabu hiyo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad