HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 27 January 2019

BENKI YA CRDB YASHEREHEKEA MIAKA 21 YA UONGOZI WA DKT. CHARLES KIMEI

 
Mwenyekiti wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei picha yenye muonekano wa mfano wa funguo ya gari ya kisasa aina ya Land Cruiser ambayo ni moja ya zawadi kwake kwa utumishi wake katika Benki hiyo kwa miaka 21. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela. Hafla hiyo ilifanyika Januari 26, 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es salaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya picha, Dkt Charles Kimei alizopicha na Marais wa awamu ya tatu mpaka ya nne pamoja na Marais wa Zanzibar na Burundi, katika dhifa ya chakula cha jioni ya kumuaga Dkt Charles Kimei aliyestaafu hivi karibuni baada ya kuitumikia Benki ya CRDB kwa miaka 21. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, Mke wa Dkt. Kimei Mama Rose Kimei (katikati) pamoja na Mama Sekita Nsekela. Hafla hiyo ilifanyika Januari 26, 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es salaa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, akielezea moja ya picha wakati wa makabidhiano hayo.
Dkt. Charles Kimei akitoka hotuba yake pamoja na kutoa shukrani zake kwa Benki ya CRDB kwa kufanya nao kazi kwa kipindi chote cha miaka 21.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla hiyo ya kumuaga mtangulizi wake, Dkt. Charles Kimei, ilifanyika Januari 26, 2019 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es salaa. 


No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad