HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 2, 2019

AZAM FC KUANZA NA JAMHURI LEO USIKU MICHUANO YA MAPINDUZI CUP



Na Ripota Wetu, Zanzibar
MABINGWA watetezi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya  Jamhuri ya Pemba, mchezo utakaofanyika Uwanja Amaan, Zanzibar saa 2.15 usiku.

Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa wa michuano hiyo mara mbili mfululizo, kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi kwenye Uwanja wa Dimani, tayari kujiweka sawa na mtanange huo unaotarajia kuwa mkali.

Akizungumza kuelekea mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri,  Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Van Der Pluijm, alisema kuwa wanaingia na malengo ya kujaribu kutwaa taji hilo na kuendeleza rekodi nzuri waliyokuwa nayo kwenye ushiriki wao kila mwaka.

“Unapoenda kwenye michuano, hauendi tu kwa lengo la kushiriki au kujaza idadi ya timu, tunataka kushinda taji, tunapaswa kufanya hivyo kama tunavyofanya katika ligi mechi hadi mechi, tunajiandaa kila wakati hasa kujenga saikolojia na akili, hili ni jambo la muhimu sana kwa wachezaji wa Kitanzania,” alisema.

Huo utakuwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa timu hizo kukutana, mara ya mwisho kukutana ni kwenye michuano iliyopita na Azam FC kuichapa mabao 4-0, yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Bernard Arthur, kiungo Salmin Hoza, Yahya Zayd na Paul Peter.

Aidha timu hizo pia ziliwahi kukutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo mwaka 2012, na Azam FC kuandika rekodi ya kutwaa taji la kwanza kati ya manne ya Kombe la Mapinduzi, ikishinda mabao 3-1, yaliyofungwa na gwiji wa timu hiyo, John Bocco ‘Adebayor’, Mrisho Ngassa na Mrisho Ahmed aliyejifunga.

Azam FC ipo Kundi B la michuano hiyo, sambamba na timu nyingine za Yanga, Jamhuri, KVZ na Malindi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad