HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 18 December 2018

Waziri wa Afya apokea Hati ya TFDA ya Ubora wa Mifumo ya Udhibiti Dawa

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa TFDA ni Taasisi ambayo inafanya vizuri na kufanya nchi kuwa kifua mbele katika masuala ya udhibiti wa Mifumo ya Dawa katika kulinda wananchi. Mwalimu ameyasema hayo wakati akipokea Hati TFDA ya Ubora wa Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Amesema kuwa TFDA baada ya kufanyiwa tathimini na Shirika la Afya Duniani (WHO) imepanda ngazi ya Tatu ya  Udhibiti wa Mifumo ya Dawa na kuwa nchi ya kwanza kwa nchi Afrika kufikia ngazi hiyo. Ummy amesema kati asilimia 100 ni asilimia 30 ndizo zimefikia ngazi ya Tatu na zilizofikia ngazi  ya Nne ni nchi zilizoendelea. Amesema kubuniwa kwa kufanyika kwa  tathimini taasisi za udhibiti duniani ili ziwe na mifumo inayowezesha kudhibiti dawa inayopaswa na hivyo kuhakikisha dawa zinazosambazwa kwenye soko na zilizo bora, salama na zinazotibu watu.Aidha amempongeza TFDA kwa hatua waliyofikia katika kuweka Tanzania kwenye ramani kwa kufikia ngazi ya Tatu kwa nchi Afrika kuwa taasisi bora.

"TFDA ni Taasisi ambayo inafanya vizuri katika suala la udhibiti wa dawa na hiyo ni kulinda watumiaji dawa"
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu Adam amesema kuwa mchakato wa kufikia hatua hiyo ulikuwa mrefu na kuahidi kuendelea kufanya vizuri na kupanda ngazi ya Nne
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma Hati ya TFDA kufikia ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa kwa Afrika iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata Utepe ya Hati TFDA ya Ubora wa ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati hafla ya kupokea Hati ya  Mamlaka ya Chakula  na Dawa (TFDA)kufikia ngazi ya Tatu ya Ubora wa Mifumo ya Udhibiti wa Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Adam Fimbo akizungumza kuhusiana na TFDA kufikia ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TFDa wakati wa hafla ya kupokea Hati ya TFDA ya Ubora wa Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad