HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 29 December 2018

Wateja wengine 20 wa NMB washinda 100,000 kila mmoja

DROO ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', imefanyika tena kwa mara ya pili Ofisi Kuu za Benki ya NMB jijini Dar es Salaam ambapo wateja 20 wengine wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja.

Akizungumza katika droo hiyo ya pili leo, Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo alisema washindi hao 20 wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo ya pili ya shindano hilo, na wamebahatika baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.

Akifafanua zaidi Bw. Achayo alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kuibuka washindi.Droo hiyo ya pili iliyofanyika leo inakamilisha jumla ya idadi ya wateja 40 ambao hadi sasa wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja huku ikiendeshwa kwa wazi na wateja wakipigiwa simu kuarifiwa ushindi wao na baadaye fedha hiyo kuingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mshindi.

Aidha aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea.Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi za fedha, simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari iliyolipiwa ya mapumziko kwenda Dubai.
Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo akizungumza jana kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Meneja Mahusiano Selcom Sebastian Msuya akifuatilia zoezi hilo.
Meneja Mahusiano Kitengo cha Kadi, Yusuph Achayo akizungumza jana kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata' Bodi. Kushoto ni Meneja Mahusiano Selcom Sebastian Msuya na Meneja NMB Kitengo cha Kadi, Stephene Jilala (kulia) wakifuatilia zoezi hilo.
 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad