HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 6 December 2018

UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI YA AKRAM AZIZ BADO HAUJAKAMILIKA

Mshtakiwa wa  kesi ya uhujumu uchumi mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz akiwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, mdogo wa mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa keai namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yaikiwemo ya kukutwa na nyara za serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018.

Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga  amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile, kuwa kesi hiyo leo Desemba 6.2018 imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Kufuatia taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Akram  anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

Inadaiwa  kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiwa maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, alikutwa na nyara za serikali ambayo ni meno sita ya tembo yenye thamani ya dola za Marekani 45,000 sawa na Sh 103, 095,000, mali ya serikali.

Pia inadaiwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay wilayani Kinondoni, mkoani humo Akram alikutwa na nyara za serikali ambazo ni nyama ya nyati yenye uzito wa kilogramu 65, yenye thamani ya dola za Marekani 1,900 sawa na Sh 4,352,900 mali ya serikali bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapoli nchini.

Katika mashitaka ya tatu hadi la 72, kwamba siku hiyo na eneo hilo hilo, mshitakiwa huyo alikutwa na silaha aina ya Pistol bila ya kibali cha mrajisi wa silaha.

Inadaiwa katika mashitaka ya 73 kuwa, Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Oysterbay mshitakiwa alikutwa na risasi 4,092 na katika mashitaka mengine ilidaiwa mshitakiwa alikutwa na risasi 2,404 bila kuwa na kibali.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu maeneo hayo ya Oysterbay, Akram alitakatisha USD 9,018 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kujihusisha na makosa ya uhalifu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad