HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 6 December 2018

HASHIM KAMBI AWASISITIZA WASANII WA FILAMU KUZINGATIA NIDHAMU

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MSANII nguli wa tasnia ya Maigizo nchini Hashim Kambi ahimiza nidhamu iwe ni kipaumbele kwa wasanii wenye majina pamoja na chipukizi katika kukuza  tasnia hiyo.

Kambi ameeleza mikanganyiko na mienendo ya wasanii kwa sasa kuwa hairidhishi na kupelekea baadhi ya wasanii kutopewa nafasi Kwenye masoko ya nje akitolea mfano nchi za jirani kama Kenya .
Hata hivyo ameeleza utofauti kati ya Wasanii wa kitanzania na  wasanii wa Kenya kuwa suala la nidhamu linachukua nafasi kubwa hasa kwa wasanii wadogo na wakubwa na kila mtu kuheshimu kazi ya mwenzie.

Vilevile Wasanii wenye majina  kuwapa vipaumbele  wakongwe ambao wapo Kwenye tasnia kwa muda mrefu na kuona ni fursa adhim kwa wakongwe hao kuendelea kutoa mafunzo na ujuzi ili kuleta Mapinduzi sekta ya  filamu nchini.

Kwa sasa nimeshiriki filamu ya hukumu ya Msanii rammy ambayo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na janga la dawa  ya kulevya  kushamiri na kuua vijana wengi nchini na kufanya Taifa letu kuendelea kuwa na vijana ambao hawana ajira na mwisho wa siku vijana wengi kuishia kufa kutokana na kuathiriwa kwa dawa hizo.
 Msanii wa nguli wa filamu hapa nchini Hashim Kambi akizungumza na wanahabari kuhusu uzinduzi wa filamu ya Rammy Garis inayoitwa  hukumu yangu  itakayozinduliwa Desemba 15 mwaka huh katika moja ya ukumbi uliyopo City mall. leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad