HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 8 December 2018

Uhamiaji wameaza kutoa viza na vibali vya Kielektroniki


Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Idara ya uhamiaji imeanza kutoa visa na vibali vya ukazi vya kiletroniki ili kurahisha upatikanaji wa viza kwa watalipa na vibali ya ukazi kwa wageni wanaokuja Tanzania kwa madhumuni mbalimbali.
Hayo ameyasema Mtendaji wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu wa Uhamiaji Ally Mtanda  katika maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwandani yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema  kuwa utoaji wa viza na vibali vya ukazi kutarahisha uingiaji kwa wageni na watalii kwani wageni watakapofika kituo cha kuingia na kutoka nchini wataonyesha taarifa ya viza walizopewa kupitia barua Pepe zao kwa uhakiki na kisha kuruhusiwa kuingia nchini hii ni tofauti ya mfumo wa sasa kwa mteja kukaa foleni kwa ajili ya kulipia viza kupitia benki na foleni nyingine kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuingia nchini.Mtanda amesema mfumo huo ni pamoja na kuimarisha usalama kwa unatunza kumbukumbu kwa wageni na matukio mbalimbali.

Aidha katika utaratibu huo itaondoa usumbufu wageni katika vituo vya kuingia nchini na kuikoa gharama zisizo za ulazima kwani kwa kuwa idara itakuwa na taarifa sahihi za wageni kabla hawajawasili nchini.Mfumo utarahisisha ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. Tangu kuzinduliwa kwa mfumo wa viza tayari maombi ya waliopewa viza wageni 140 ambapo Tanzania Bara 89 Zanzibar 40.

41 wamewasilisha maombi hayo katika ofisi mbalimbali za uhamiaji ambapo vibali hivyo vinafanyiwa kazi.Waliomba vibali katika za Uhamiaji Makao Mkuu 32,  Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC) Watano, pamoja na EPZA watano. Tangu  kuanzishwa kwa mfumo wa hati ya Kusafiria Kieletroniki jumla ya passport 55078 zimetolewa hadi kufikia Novemba.

Afisa wa Passport Vedasto Rweikiza akimuhudumia mwananchi katika maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Idara wakitoa huduma katika Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad