HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 6 December 2018

UHAMASISHAJI WA USAFI WA MAZINGIRA WILAYA YA CHEMBA WAFANYIKA

Na Shani Amanzi
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga amewataka Wananchi wa Chemba kujali afya zao kwa kufanya usafi wa mazingira kuanzia majumbani kwao ikiwemo  kuwa na vyoo bora ili kuzuia magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindu pindu.

Mhe.Simon Odunga ameungana sambamba na Rais wa  Awamu ya Tano Mhe ,Rais John Pombe  Magufuli  na kuridhia ,Tamko la Rais la kuhakikisha kaya zote katika Wilaya  ya Chemba zinakuwa na vyoo bora.

 “Ntahakikisha kila kaya inakuwa na vyoo bora na kuvitumia  ,kwa kaya nyingine ambazo hazina vyoo naelekeza  kwa viongozi wenzangu na vijana  kama tulivyokubaliana  kuanzia 25/12/2018  kila kaya iwe na choo bora na kukitumia na kuagiza viongozi wotewanaohusika katika  ngazi zote za wilaya, Kata,Tarafa ,Vijiji na Vitongoji kusimamia kikamilifu agizo langu hili”aliongeza kwa kusema  hivyo Mhe.Simon Odunga.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus  Mashimba ameipongeza Wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   na Msanii Mrisho Mpoto  kwa kuwa na ubunifu wa uhamasishaji ,kwani wilaya  ya Chemba wameitika kwa mwitikio mkubwa na kupokea ujumbe huo.

 Aidha Dkt.Mashimba amesema  “katika taarifa ya ya robo mwaka July,September jumla ya kaya 60,576 zilitembelewa kati ya hizo kaya zenye vyoo vya muda ni 47,487  sawa na asilimia 78.4 na kaya zenye vyoo vya kudumu ni 11,920 sawa na asilimia 19.7 na changamoto iliopo ni baadhi ya jamii kutoezeka  vyoo vyao,kwa imani ya kuogopa nyoka kuingia kwenye vyoo”
Naye Msanii Mrisho Mpoto amesema katika kampeni hii aliyoshirikiana na Wizara ya Afya ya kusema”Usichukulie Poa Nyumba ni Choo”wameweza kuzunguka Kata 10 ikiwemo Mondo,Jangalo,Goima ,Mrijo,Babayu,Kidoka ,Soya,Gwandi,Kelema na Chemba  wamefarijika sana kwani mwitikio wa wananchi ni mkubwa  bali kata moja tu ambayo ni ya Babayu imeonekana ina idadi kubwa ya kaya zisizo na vyoo.

Hata hivyo sheria ndogondogo za Halmashauri zinaendelee kutumika katika kuwabana wasio na vyoo pamoja na wasiokamilisha ujenzi wa wa choo bora,aidha kampeni hiy ya uhamasishaji wa mazingira imehitimishwa katika kata ya Chemba ambapo kampeni hiyi ilifanyika ndani ya siku tano kuanzia Tarehe 1 mpaka5/12/2018 ilipomalizika katika uwanja wa Godown,Chemba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad