HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 24, 2018

TTB NA CHINA KUSHIRIKIANA KUUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA NCHINI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SERIKALIya Nchini China imedhamiria kuisaidia Bodi ya Utalii nchini (TTB) katika kutangaza vivutio mbalimbali nchini na kukuza biashara kati ya nch hizo mbili Tanzania na China.






Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa lengo kuu la ziara iliyofanyika nchini China katika Jiji la Shanghai, Guangzhou, Hong Kong, Chengdu na Beijing Novemba 12-20 ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza utalii.

Amesema, wametumuia fursa hiyo kuhakikisha Tanzania inaongeza sehemu ya umiliki wa soko kwenye soko la utalii kwa kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zikizopo nchini ikiwamo na safari za ndege za ATCL kwenda China.

Jaji Mihayo ameeleza kuwa, katika safari hiyo ya nchini China wameweza kusaini mkataba na kampuni ya Touchroad Group na TTB na wamekubaliana kuwa kampuni hiyo italeta watalii elfu kumi (10,000) kutoka China hadi kufikia mwaka 2019.

"Kundi la kwanza la watalii wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi Januari na Februari 2019, watakuwa nchini kwa muda wa siku tatu na Touchroad wameonesha nia ya kuwekeza katika huduma ya malazi zenye hadhi ya nyota tano na tayari wanazo hoteli nne,"amesema Mihayo.

Katika ziara waliyoifanya ya jiji la Beijing, wawakilishi wa Shirika la Utangazaji la China (CCTV) walikutana na maafisa wa MNRT na wakatoa mapendekezo ya kutengeneza makala za dakika 30 za Zamadam kisha kutoa Filamu kama ya Jurassic Park ili kurushwa kwebye televisheni yao.

"Pia, CCTV4 wameafiki kushiriikiana na Bodi ya misitu nchini (TFS) kupiga picha katika hifadhi za asili za misitu wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa China mnamo mwezi Februari 2019,"amesema Jaji Mihayo.

Aidha, amesema kuwa kwa takwimu inaonesha Tanzania kwa mwaka 2017 imeweza kupokea watalii 29,224 kutoka nchini China wakitembelea vivutio tofauti nchini.

Kwa upande wake, Meneja Mauzo na Usambazaji wa ATCL, Edward Nkwabi alisema kuwa katika ziara hiyo walipokea maombi kutoka kwa viongozi wa miji ya Hong Kong, Beijig, Chengdu na Shanghai kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi kwenye miji hiyo.

Alisema, jambo hilo liliwafanya kuingia makubaliano na kampuni moja ya uwakala ambayo itatangaza na kuuza tiketi za safari za ndege za ATCL. 

Amesema kwua safari za moja kwa moja kuelekea nchini China zitaanza mapema mwakani kwa ajili ya kuimarisha sekta ya utalii nchini na lengo kuu ni kuwapa fursa ya kuja moja kwa moja kutoka China hadi Tanzania.

Mwakilishi kutoka ubalozi wa China, Gao Wei alisema kuwa kupitia ziara waliyoifanya TTB, ATCL, Wizara ya utalii pamoja na wadau wengine wakiwemi wamiliki wa Hoteli, Serikali ya China imeendelea kukuza na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania nchini China.

Amesema, Tanzania wana vivutio vingi sana na wao kama serikali ya China wanaona hii ni fursa kwao ila wametoa pendekezo moja kwa TTB kuweza kuondoa Viza ili watalii wengi waweze kuja na suala hilo tayari wameshawaeleza na wanaamini watalifanyia kazi.
MWENYEKITI wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji mstaafu Thomas Mihayo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya ziara kutangaza utalii katika soko la utalii la China. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devota Mdachi na kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa ATCL, Edward Nkwabi akizungumzia maombi kutoka kwa viongozi wa miji ya Hong Kong, Beijig, Chengdu na Shanghai kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi kwenye miji hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad