HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 24 December 2018

DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HIINa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

DROO ya  upangwaji wa Makundi hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF) inatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa Disema 28 ili kupata makundi manne yatakayoanza kuchuana Januari 16 mwaka huu  makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.Timu hizo zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 baada ya kufanikiwa kushinda mechi zao za mzunguko wa pili na kutoka Afrika Mashariki na kati timu pekee kutoka Tanzania Simba wamefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuwafungwa Nkana 'Red Devil' goli 3-1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 2-1 wakiwa ugenini.

Katika uchezeshaji wa droo hiyo timu ya Simba imewekwa katika kundi cha nne kutokana na nafasi ya kisoka kwa klabu za Afrika na watasubiri timu zitakazoanza kupangwa kutoka kundi la  kwanza hadi la tatu.


Mbali na Simba SC, timu nyingine zilizofuzu Ligi ya Mabingwa Afrika ni mabingwa watetezi, Esperance na Club Africain zote za Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Ismailia, Al Ahly za Misri.


Timu zingine TP Mazembe na AS Vita za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Wydad Casablanca ya Morocco, JS Saoura, CS Constantine za Algeria, Horoya FC ya Guinea, Lobi Stars ya Nigeria, FC Platinums ya Zimbabwe na ASEC Mimosa ya Ivory Coast.


Mara ya mwisho Tanzania kuingiza timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka 2003 na walikuwa hao hao Simba SC waliofika hatua hiyo, wakifuata nyayo za wapinzani wao wa jadi, Yanga SC waliokuwa timu ya kwanza nchini kufikia mafanikio hayo mwaka 1998. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad