HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 21 December 2018

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA UWT ZANZIBAR APOKELEWA KWA SHANGWE

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu mpya wa Zanzibar wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT), Tunu Juma Kondo, amesema atahitumikia jumuiya hiyo kwa hekima na busara ili kutimiza kwa vitendo malengo ya CCM na Jumuiya hiyo.

Amesema baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ametambua kuwa siasa ni hekima na busara hivyo katika utendaji wake atafanya kwa misingi hiyo kwa uadilifu mkubwa.

Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na wanajumuiya wa UWT katika ukumbi wa CCM kisiwandui,Naibu huyo alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo na kwamba utaratibu wa chama ni mzuri wa kuwateua viongozi bila ya ubaguzi.
Katika maelezo yake Naibu huyo alisema CCM haina ubaguzi na kwamba inazingatia utendaji wa mtu na si vinginevyo akitoa mfano alisema kwa upande wake hakutarajia kuwa siku moja atapewa jukumu kama hilo.

"Nashukuru UWT kwa kuridhia jina langu lipelekwe katika uongozi wa juu wa chama hivyo sina budi kuwashukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM,Dk.Bashiru Ally,kamati ya Halmashauri Kuu kwa kuniamini na wameonesha imani kubwa kwangu,"alisema Naibu Katibu Mkuu huyo Tunu aliwataka wanajumuiya hiyo kumpa ushirikiano katika utendaji wake na amewataka wakumbuke kuwa siku za mbele kuna uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kwamba wao ndio wapiganaji hivyo wanapaswa kushirikiana.

"Naomba tushirikiane kwa karibu kutokana na kuwa ushirikiano wetu ndio nguzo ya utendaji katika kuwasemea wanawake wenzetu na watoto wetu ninaomba sana ushirikiano wenu kwani nyinyi wanajumiuya ndio mmenifanya kuwa Naibu Katibu Mkuu,"alisema 

Kwa upande wake Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi,Mgeni Hassan Juma alisema anashukuru Mwenyekiti wa Taifa CCM,kwa kumteua kuwa Naibu Katibu Mkuu na kwamba uamuzi alioufanya ni sahihi.

Alisema Naibu huyo anatosha katika nafasi hiyo na kwamba akiwa mwanamke wanamatarajio makubwa katika jumuiya hiyo kutokana na uwezo wake wa kiutendaji wa muda mrefu ndani ya UWT.

"Tunamuelewa sana uwezo wake katika utendaji wake wa kazi na kwamba ni mstaarabu,mvumilivu na ana hekima hivyo kwa kipindi kirefu amekuwa akikaimu nafasi hiyo na amefanya kazi za siasa ndani ya jumuiya,"alisema Naibu Spika huyo

Katika maelezo yake aliongeza kuwa Tunu amefanya mambo mengi ndani ya jumuiya hiyo ikiwemo amesimamia uchaguzi wa jumuiya kwa usalama hivyo wanajumuiya ya wanatarajia Naibu Katibu Mkuu huyo kusimamia kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 kwa uweledi mkubwa.

Naye Mwakishi wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Hidaya Ali Makame, amesema kwamba Naibu Katibu Mkuu huyo amekuwa ni kiongozi asiyejikweza anayefanya kazi na wanachama wa ngazi zote ndani na nje ya chama hicho.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akivishwa koja la Ua ikiwa ni ishara ya mapokezi yake mara baada ya kuwasili kisiwanduzi Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM Zanzibar  Khadija Kabir mara baada ya kuwasili Zanzibar  kwa mara ya kwanza toka alipoteuliwa kushika nafasi hiyo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akifurahia na wanachama wa UWT katika mapokezi hayo.
  NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akizungumza na wanajumuiya wa UWT katika ukumbi wa CCM Kisiwandui

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad