HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 23 December 2018

Mbunge Zungu azinduwa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga, Ilala

MBUNGE wa Ilala, Mussa Azzan Zungu amezinduwa rasmi kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation ikiwa ni kuhamasisha uzalendo kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kauli ya Juni 21, 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Mbunge Zungu aliwataka wananchi wa Ilala kutumia huduma za TTCL ili kukuza uchumi wa Tanzania moja kwa moja kutokana na faida zinazopatikana kutumika kuleta maendeleo kwa jamii.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (katikati) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (kulia).
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (wa tatu kushoto) pamoja na Meza kuu wakionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Katika tamasha la burudani lililoandaliwa na TTCL Corporation na kufanyika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala kuhamashisha matumizi ya huduma na bidhaa za Shirika la TTCL.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na baadhi ya wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala, Uwanja wa Karume.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala, Uwanja wa Karume wakifuatilia burudani.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala, Uwanja wa Karume wakifuatilia burudani.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga wilaya ya Ilala. Wengine ni viongozi meza kuu.
Baadhi ya wacheza shoo wakiwaburudisha wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo.
Msanii nguli Dully Skykes akiwapagawisha mashabiki wake katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga, Wilaya ya Ilala.
Mkongwe Dully Skykes akiimba na mashabiki kwenye kampeni hizo.
Shishi Baby aka Shilole akikimbiza katika kampeni hizo zilizofanyika uwanja wa Karume.
Msanii Shilole akimwaga mauno jukwaani.
Mtaalam wa ngoma za Kisingeli, Man Fongo akiwaimbisha 'masela' kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad