HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 7, 2018

KLINIKI YA BIASHARA IPO TAYARI KUTOA HUDUMA, TAGLA YAHAIDI USHIRIKIANO KUKUZA VIWANDA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAONESHO ya tatu ya bidhaa za viwanda vya Tanzania na siku ya viwanda Afrika yamezinduliwa rasmi yakiwa na kauli mbiu ya  "Sasa Tunajenga Tanzania ya Viwanda" huku matumizi ya teknolojia katika kutafuta masoko ndani na nje ya nchi yakisisitizwa.

Akifungua maonesho hayo Naibu waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano imejizatiti katika kuhakikisha mpango kazi wa kuyafikia maendeleo unafanikiwa na kufikia 2025 wananchi wote wawe na vipato vya kati.

Aidha amesema kuwa uhakika wa masoko kwa bidhaa zinazozalishwa ni muhimu sana hasa kwa kutangaza bidhaa hizo ndani na nje kupitia maonesho ya aina hiyo.

Aidha amezipongeza taasisi 513 zilizoshiriki maonesho hayo na kuahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya viwanda itaendelea kuratibu na kuunganisha sekta zote katika kuhakikisha sekta hiyo inakua imara zaidi.

Pia amewataka wafanyabiashara watumie kliniki ya biashara iliyoanzishwa kwa kupeleka kero zao ili ziweze kutatuliwa na amewataka maafisa biashara ya Halmashauri na Wilaya kusikiliza kero za wafanyabiashara na kuziwakilisha mahala husika.

Vilevile Manyanya ameitaka wakala  wa mafunzo kwa njia ya mtandao (TAGLA) kuwasaidia wafanyabiashara kupitia teknolojia kutangaza bidhaa hizo ndani na nje ya nchi kama wafanyavyo kwenye mikutano mengine ya ujifunzaji, pia ameshauri kuweka huduma hiyo kwenye ofisi mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao charles Senkondo amesema kuwa, huduma zitolewazo na wakala hiyo zitasaidia sana katika kukuza ukuaji wa viwanda nchini hasa kwenye kutafuta masoko nje ya nchi.

Senkondo amesema kuwa mawasiliano ni muhimu hasa katika kuwashirikisha washiriki ili kuweza kufikia malengo, na kwa matumizi ya teknolojia hiyo malengo yatafikiwa  kwa urahisi zaidi na watu wengi wataweza  kutangaza  bidhaa za Tanzania ulimwenguni kote kwa njia ya mtandao.

Senkondo amesema kuwa wao kama wakala wapo tayari katika kushirikiana na wafanyabiashara na wenye viwanda katika kutangaza bidhaa za Tanzania ili kuweza kufikia azma ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini (TANTRADE) Edwin Rutageruka amesema kuwa jukumu la mamlaka hilo sio kuandaa maonesho pekee bali kutafuta masoko kwa bidhaa zinazozalishwa na wanaendelea kutekeleza jukumu hilo na kuhakikisha bidhaa hizo zinauzika na changamoto zinapatiwa uvumbuzi.

Rutageruka amewataka wafanyabiashara na wenye bidhaa kutumia fursa hizo za kuonesha bidhaa zao katika maonesho kama hayo sambamba na kutumia kliniki ya biashara kwa kuwasilisha changamoto zao hasa za masoko na kupata ushauri wa kibiashara.
 Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akisalimia na wajasiriamali wanaoshiliki maonesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
 Kulia  Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja wa Shirika la bima la taifa (NIC), Elisante Maleko akitoa maelezo ya bima ya kilimo kwa Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya  ambapo akitoa wito kwa wakulima ote nchini  kujiunga na bima ya Taifa katika  maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji,Mhandisi Stella Manyanya akisalimia na Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja wa Shirika la bima la taifa (NIC), Elisante Maleko leo alipotembelea banda la (NIC) katika maonyesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo  funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji,Mhandisi  Stella Manyanya akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao,Charles Senkondo alipotembelea banda la banda hilo katika maonesho ya tatu ya bidhaa za wiwanda vya hapa nchini yaliyo funguliwa leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa mafunzo kwa njia ya mtandao Charles Senkondo wakiangalia namna ya kufanya mkutano kwa njia ya mtandao leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye banda la NIDA ndani ya maonyesho ya Tatu ya Bidhaa za viwanda wakipatiwa elimu juu ya zoezi la usajili, umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa na taratibu za kufuata ili kukamilisha hatua za awali za usajili.Picha na Emmanuel Massaka wa MMG) Naibu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya aliyeambatana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara,Edwin  Rutageruka, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino – NIDA Bi. Rose Joseph, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ndani ya maonyesho Tatu ya Bidhaa za Viwanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad