HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 29, 2018

Zaidi ya wahitimu 297 wamehitimu katika Chuo cha VETA Kihonda

Zaidi ya wahitimu wapatao 297 katika chuo cha VETA Kihonda wamehitimu mafunzo yao katika fani mbalimbali miongoni mwao wavulana 49 na wasichana 248,mahafali hayo yalifanyika  katika chuo cha VETA Kihonda mnamo tarehe 23,November 2018,Mahafali hayo yaliuzuriwa na Mgeni rasmi ndugu Beda Marwa Mjumbe wa bodi ya VETA kanda ya mashariki.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo aliyekuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo ndugu Beda Marwa ambaye ni Mjumbe wa bodi ya kanda ya Mashariki aliwaomba wanafunzi watumie vizuri elimu waliyo pata ya Ubunifu kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ili kushindana na mafundi wengine walio wazoefu.

Alisema taifa linatambua umuhimu wa kuwepo kwa Vyuo vya Ufundi Stadi vyenye kuwaandaa wataalamu katika nyanja mbalimbali za ufundi.  Alisema Vyuo hivi ni sehemu muhimu ya kuwaandaa vijana kukabiliana na soko la ajira, na vijana kupata ujuzi wa kujiajiri wao wenyewe.

Marwa aliwaomba wanafunzi kutambua ya kwamba kazi nyingi za mafundi ni kazi zinazoonekana kwa kila mtu hivyo kama watakuwawanafanya vizuri kazi zao na kwa kiwango cha juu kizuri tayari inaweza kuwa ni  sehemu mojawapo ya kujitangaza na kujipatia ajira binafsi kwa urahisi zaidi.
Naye Mkurugenzi wa VETA kanda ya Geofrey Sabuni aliwapongeza vijana kwa kufikia hatua nzuri kimaisha ya kumaliza masomo yao katika chuo cha VETA Kihonda na kuwashauli kwenda kuwa mabarozi wazuri huko mtaani waendako katika kuitangaza VETA.
Mr.Sabuni alisema jukumu kwabwa la VETA ni kuhakikisha wanawaandaa wanafunzi kuwa mafundi bora katika ujenzi wa taifa,
Aliongeza kwa kusema  VETA wanajitahidi katika kuhakikisha tunaandaa watu mahili wa kufanya kazi kwa kuhakikisha wanaa andaa mitahara inayo endana na mabadilioko ya soko la ajira kwa kuhakikisha vyuo vya VETA vinakuwa na  ,walimu wa kutosha,pomoja na Vitendea kazi mazubuti.
Naye kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kihonda ndugu Kashindye k.Maganga alisema nimatarajio ya Chuo kutokana na mafunzo waliyoyapata wahitimu, wanatarajia watakuwa wabunifu, waangalifu,waaminifu,hodari na watakuwa tayari kujiendeleza kwa mafunzo ya ngazi nyingine za masomo.

aliongeza kwa kusema katika kuhakikisha wanawafikia Vijana wengi zaidi hasa katika fani zile zenye huitaji zaidi chuo kimeanzisha program ya wanafunzi wa mchana (Evening Class) katika fani za umeme wa magari, umeme wa majumbani, ufundi wa magari, ufundi wa bomba na ukerezaji wa vyuma.

Maganga alisema “chuo kimeweza Kuongezeka udahili kwa wafunzi wa kozi ndefu na fupi, kutoka idadi ya wanafunzi 480 hadi 600 kwa kozi ndefu na kutoka wanafunzi 970 hadi 1,200 kwa kozi fupi kwa mwaka”.

Maganga alichukua fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuweza kuwapatia vifaa mitambo ya kisasa ya  kufundishia katika fani ya Kilimo (Agro-Mechanics) na kuhahidi kuvitumia kwa uhangalifu lakini pia kuitumia kufanya uzalishaji wa mazao mbali mbali katika chuo hicho pamoja na kuwafundishia wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad