HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 29, 2018

WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO

Na Frankius Cleophace Mara
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto. Ummy Mwalimu  amemuagiza katibu mkuu wa afya kuhakikisha kila Hospital za Rufaaa za Mikoa  yote Tanzania  kuwa na vifaa tiba  vya kinywa na meno kabla  ya machi 30, 2019.

Kauli hiyo imetolewa wakati akifungua mkutano wa madaktari bingwa wa kinywa na meno Tanzania katika ukumbumbi wa mwekezaji wa mkuu wa mkoa wa Mara. Waziri ummy amesema kuwa kufanya hivyo nikuhakikisha wanaondoa changamoto katika hospital zote nakuowaondolea wananchi usumbufu  wanaoupatapa kipindi wakitembea  zaidi ya kilomita 200 kuitafuta huduma ya kinywa na meno.

Pia amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawahudumia na kuwajali wananchi wote nakuhakikisha wanapata huduma zote katika maeneo yaliyokaribu nao ambapo amewakikishia Madaktari bingwa kuanzia hospital za wilaya katika mkutano ujao itakuwa tayari wameshatekeleza adhima hiyo. Naye mkuu wa Mkoa wa Mara Adamu Malima amewapongeza madkatari Bingwa wa kinywa na meno kwa kuupa kipaumbele Mkoa wa Mara katika utaoji wa huduma hiyo huku akimuomba waziri kuangalia namna ya kusaidia wananchi wa mkoa huo katika utoaji wa huduma hiyo.

Awali akitoa Taarifa mbele ya waziri wa Afya Rais wa madaktri wa kinywa na meno Ambege Mwakatobe amesema kuwa pamoja na jitihada zao zote wanakwamishwa na changamoto ya upungufu wa watalamu wa kinywa na meno ambapo baadhi ya maeneo Nchini Tanzania yanakosa upatikanaji wa huduma hiyo  pia hakuna chuo ambacho kinafundisha wahudumu hao wa kinywa na meno. Zoezi la kuendelea kutoa huduma ya tiba ya kinywa na meno kwa baadhi ya Maeneo katika wilaya za Mkoa wa Mara zinaendelea ili kuweza kuwanusuru wagonjwa wa Meno.
 Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza na madaktari katika mkutano wa madaktari bingwa wa kinywa na Meno uliofanyika katika ukumbi wa Mwekezaji Mkani Mara.
  Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima akiongea na madaktari hao katikati ni Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu na wakwanza kulia ni Rais wa madaktri wa kinywa na meno Ambege Mwakatobe.
 Rais wa madaktri wa kinywa na meno Ambege Mwakatobe  akizungumza katika mkutano huo.
 Daktari Merina Njelekela ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi  akiongea katika Mkutano huo wa madakri bingwa wa kinywa na Meno uliofanyika mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad