TFF YATANGAZA UCHAGUZI WA YANGA KUFANYIKA JANUARI 13 2019 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 5 November 2018

TFF YATANGAZA UCHAGUZI WA YANGA KUFANYIKA JANUARI 13 2019

 Mwenyekiti wa kamati  ya Uchaguzi ya TFF , Ally Mchungahela akizungumza na waandishi kuhusiana na uchaguzi wa klabu ya Yanga.


Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi maalum wa kujaza nafasi ambazo zilizo wazi ndani ya klabunya Yanga ikiwemo ile ya Mwenyekiti.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Mchungahela amesema zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea litaanza Novemba 8 hadi 13 2018 na wanachama wote watatakiwa kuhakiki majina yao kwenye matawi.

Aidha ameeleza kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 13 2019. TFF wamemua kutangaza rasmi kuanza mchakato huo mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuwataka wausimamie wakieleza kuwa kamati ya Yanga haijitoshelezi.

BMT waliitaka TFF itimize majukumu hayo katika kikao na wanahabari kilichofanyika siku chache zilizopita.

BMT  iliiwataka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojizuru huku ikiwemo ya Manji aliyeiandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Klau hiyo
Taarifa ya BMT kwa vyombo vya Habari ilisema kwamba, Yanga imebaki na Wajumbe wanne kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.

Viongozi waliojiuzulu ndani ya klabu hiyo ni Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, na wajumbe Hashimu Abdallah, Salum Nkemi, Omary Said, Ayoub Nyenzi na huku waliobaki ni wajumbe Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay, Siza Lyimo na Hussein Nyika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad