HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 5 November 2018

TAMASHA LA WASAFI FESTIVAL KUZINDULIWA RASMI NOV 24 MTWARA


Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul 'Daimond Platinumz'  akizungumza na waandishi wa habari wakati wakutambulisha rasmi tamasha la Wasafi Festival Nov 24 mwaka huu Mkoani Mtwara.


Na Khadija Seif,Globu ya Jamii

Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul maarufu kama Daimond Platinumz ametangaza ramsi kuanza kwa tamasha la Wasafi Festival Novemba 24 mwaka huu.


Tamasha hlo linalotarajiwa kufanyika kwenye mikoa mbalimbali nchini litaanzia Mkoani Mtwara ikiwa ni mara ya kwanza toka kuanza kwa Tv na Redio.


Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari  Leo Jijini  Dar es salaam, Diamond  amesema kuwa tamasha la Wasafi Festival lina lengo la kutoa burudani nchini na nje ya nchi ili kutangaza mziki wa kitanzania zaidi na kufundisha jamii jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri.

Diamond amesema kuwa, licha ya kutangaza mziki huo kwenye mikoa ambayo itapata kushuhudia burudani hiyo ni wataanzia tarehe 24 mwezi huu kwenye mkoa wa Mtwara katika viwanja vya Nangwanda na ikifatiwa na mkoa wa Iringa,Morogoro , Zanzibar na mikoa mingine na pamoja na nchi ya Kenya.

Amefafanua zaidi katika kila Mkoa utakaotembelewa pia watapata fursa kwa  kukarabati shule , Wanafunzi kupatiwa sare za shule, madaftari na kupatiwa madawati huku kwa wakina mama wasiopungua 200 kupewa mitaji ya kibiashara ili kujikwamua kiuchumi .

Sambamba na hilo wasichana wasiopungua 20 watapewa mafunzo ya urembo wa uso pamoja na vifaa vya kupambia. 


Meneja wa msanii Daimond Platinum Hamis Tale maarufu kama Babu Tale amewaambia wazi kwa sasa radio ya wasafi iko hewani kupitia masafa ya 88.9 ambayo ipo kwa ajili ya kutoa fursa kwa ambao vipaji vyao havijapata nafasi ya kuvuma.

Tale ametoa rai kwa mashirika ,wadau na wanamuziki ambao wangependa kushiriki katika tamasha hilo nafasi zipo wazi wanakaribishwa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad